Meza kuu ya viongozi wa Jumuiya ya Ahmadiyya pamoja na Afisa maendeleo ya jamii kabla ya kukabidhi msaada katika kituo cha Yatima Songwe |
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Mbeya, Bevarine Mgoda akizungumza na watoto kabla ya kukabidhi msaada |
Kiongozi wa wazee wa Jumuiya ya Ahmadiyya Mkoa wa Mbeya, Hafidhu Mgagi akimkaribisha Shehe mkuu kuzungumza na watoto kabla ya kukabidhi misaada |
Shehe Mkuu wa Kanda ya Mbeya wa Jumuiya ya Kiislamu ya Ahmadiyya akizungumza jambo na watoto wanaolelewa katika kituo hicho |
Watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima kilichopo Songwe wakisikiliza kwa makini |
Viongozi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Ahmadiyya wakikabidhi misaada mbali mbali kwa walezi wa kituo cha Yatima Songwe Mbeya |
Watoto wakiwa pamoja na baadhi ya vitu walivyokabidhiwa na jumuiya ya Ahmadiyya Mbeya |
KATIKA kuhitimisha mfungo wa mwezi
mtukufu wa Ramadhani, Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya, Mkoa wa Mbeya imefanya
ziara ya kutembelea vituo vya watoto Yatima na watoto wi moja wenye mahitaji
maalumu.
Ziara hiyo ilifanyika juzi ambapo
viongozi wa Jumuiya hiyo wakifuatana na Shehe mkuu wa Kanda ya Mbeya,
Karim-Ud-Din Shams walitembelea kituo cha Malezi na Mafunzo ya Watoto Yatima
Good Samaritan Orphanage Trust kilichopo Songwe Wilaya ya Mbeya mkoani hapa na
kutoa msaada wa bidhaa mbali mbali.
Akimkaribisha Shehe Mkuu kukabidhi
zawadi hizo, Kiongozi wa baraza la Wazee wa Jumuiya ya Ahmadiyya Mkoa wa Mbeya,
Hafidhu Mgagi, alisema Waumini wa dini ya Kiislamu duniani kote wako kwenye
mfungo wa mwezi wa Ramadhani ambao uko ukingoni kuisha, hivyo Jumuiya hiyo
imeona ni vema ikashiriki na Yatima katika sikukuu ya Idi.
Kwa upande wake Shehe Mkuu wa Kanda ya
Mbeya inayounda mikoa wa Mbeya, Rukwa na Katavi, Karim Shams alisema kutembelea
Yatima ni moja ya maandiko matakatifu ya Mungu yanayomtaka kila mwislamu
kuwajali watoto Yatima na wasiojiweza ili waweze kupata thawabu.
Alisema lengo la kutembelea kituo hicho
ni kusherekea na watoto sikukuu ya Idd itakayofanyika hivi karibuni baada ya
kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuongeza kuwa hayo ni moja ya
matakwa ya maagizo ya dini ya kushirikiana na yatima ili kupata thawabu siku ya
kiama.
Katika hafla hiyo Jumuiya hiyo ili
kabidhi bidhaa mbali mbali zikiwemo Sukari, Mchele, mafuta ya kupikia na sabuni
za kufulia ambazo thamani yake haikujulikana mara moja kutokana na kugawanywa
katika sehemu zingine zenye mahitaji.
Kwa upande wake Mlezi wa Kituo hicho,
Yusufu Salali, alitoa shukrani kwa Jumuiya hiyo kwa kuwajali watoto wanaolelewa
katika kituo hicho licha ya kumulikiwa na dini ya kikristu lakini Waislamu
hawakufanya ubaguzi na kutoa misaada bila kujali udini.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya jamii
Wilaya ya Mbeya,Bevarine Mgoda, alisema sula la watoto yatima katika Wilaya
yake linakabiliwa na changamoto nyingi hivyo alitoa shukrani kwa wadau
kuendelea kuwajali zikiwemo taasisi za serikali na sio kuiachia Serikali pekee.
Alizitaja baadhi ya Changamoto hizo kuwa
ni pamoja na ufinyu wa usafiri wa kuweza kuwatembelea watoto yatima popote
walipo hatan kushughulikia maswala yao yanapojitokeza kwa ghafla hususani
vijijini ambako vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ni vingi.
Aliongeza kuwa changamoto nyingine ni
ukosefu wa elimu kwa wanajamii ambao kutokana na hali hiyo wamekosa uzalendo wa
kuona kila mtu anaweza kuhudumia mtoto yatima bila kujali katika katika familia
ya aina gani.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment