Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, June 20, 2014

ANGALIZO: WACHINA WAVAMIA JIJINI MBEYA NA KUUZA SIMU WANAZO DAI KUWA ORIGINAL WAKATI NI FEKI. WAHUSIKA MPO?

 Mwandishi na Msimamizi Mkuu wa Mbeya Yetu Blog Joseph Mwaisango akiwa anashuhudia Simu hizo Feki na ambazo ukiziangalia kama mzoefu utajua ni Original , Simu hizo ni kama Samsung Galaxy na zenginezo .
Akiendelea kumuuliza maswali Mchina huyo. 

Jijini Mbeya katika maeneo mbalimbali likiwemo eneo la Soweto kumeibuka biashara ya hawa wanaowaita wawekezaji wachina ambao wamevamia jiji na kufanya biashara ya Simu bei poa ambazo kwa kuziangalia kwa macho utasema ni Original na kumbe ni Feki, Simu hizo mbalimbali ambazo ukizikuta dukani kabisa na zenye bei kali kuanzia milioni  au Laki tisa na zaidi wao wanauza laki tatu tuu, na watu  wengi wamesha ingizwa mjini bila kujua. 

Swali linakuja Je Serikalini wahusika wanalitambua hili linalo endelea na kama ndio wanalijua je wamewachukulia hatua zipi na huu ndio uwekezaji?

Kuweni makini epukeni kutapeliwa!

No comments: