Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, May 13, 2014

Wilaya ya Chunya inatarajia kutumia zaidi ya shilingi Bilioni 48 katika bajeti ya mwaka 2014/2015

 Kaimu Mkurugenzi  wa Halmashauri ya wilaya Chunya Charles Mwakalila alipokuwa akiongea na mwandishi wa Mbeya yetu ofisini kwake hivi karibuni.


Ofisi za Halmashauri wilaya ya Chunya

Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro amewataka wananchi kuwekeza katika wilaya hiyo kwani hivi sasa imepiga hatua katika mawasiliano ya simu na barabara kuu ya Chunya/Mbeya inayojengwa kwa kasi kubwa.
Chunya yazidi kujengeka kwa kasi

Ujenzi wa barabara waendelea kwa kasi




Barabara ya kuelekea chunya maeneo ya Kiwanja


Chunya yazidi kukua kimaendeleo

Wilaya ya Chunya inatarajia kutumia zaidi ya shilingi Bilioni 48 katika bajeti ya mwaka 2014/2015 kwa miradi ya huduma na maendeleo.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya  Charles Mwakalila alipokuwa akiongea na mwandishi wa Mbeya yetu ofisini kwake hivi karibuni.

Baadhi ya miradi iliyopewa kipaumbele ni miradi ya maji,elimu,miundo mbinu ya barabara na ujenzi wa uwanja wa michezo utakaogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 8.2.

Mwakalila amesema kuwa mapato ya Bajeti hiyo yatatokana na vyanzo mbalimbali kama vile tumbaku,kilimo madini na ruzuku kutoka serikalini.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro amewataka wananchi kuwekeza katika wilaya hiyo kwani hivi sasa imepiga hatua katika mawasiliano ya simu na barabara kuu ya Chunya/Mbeya inayojengwa kwa kasi kubwa.

Na Mbeya yetu

1 comment:

Anonymous said...

Tutasubiri mkamilishe hivyo vipaumbele vyenu maana wewe si wakwanza kutamka. Maji ni tatizo kubwa sana chunya (mf. Makongolosi). miundo mbinu yake ni ya zamani sana.