Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, May 9, 2014

MASTALA CUP KUTIMUA VUMBI MBEYA

Meneja usambazaji wa Kampuni ya Cocacola kanda ya Nyanda za juu kusini, Emmanuel Mnyoga, alisema wanajisikia fahari kusaidia kuinua vipaji vya michezo kuanzia ngazi za chini kupitia udhamini wanaoutoa.

Mratibu wa mashindano ya Mastala Cup Willy Mastala akisoma ratiba ya mashindano hayo ambayo yanatarajia kushirikisha jumla ya timu 20 katika Viwanja vya Mwenge Jijini Mbeya.


Meneja Mauzo Kampuni ya Coca Cola Kanda ya Mbeya Jayanti Vekaria akielezea namna ambavyo kampuni hiyo imefanikiwa kuibua vipaji vya wanasoka kupitia mashindano mbaalimbali yanayodhaminiwa na kampuni hiyo.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwasikiliza waandaaji wa mashindano hayoRashid Mkwinda akiuliza swali wa wadhamini haoAdd captionLIGI ya Mpira wa miguu ya Kombe la Mastala linatarajia kuanza kutimua vumbi Mei 10, Mwaka huu katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Mtenda ilioyopo Soweto jijini hapa, Mratibu wa Ligi hiyo, Willy Mastala alisema jumla ya timu 20 zimethibitisha kushiriki ligi hiyo.

Mastala aliongeza kuwa ligi hiyo imedhaminiwa na Kampuni ya Soda ya Cocacola Kwanza Mbeya kwa udhamini wa shilingi Milioni Tano zitakazotumika kutoa zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu.

Alizitaja zawadi hizo kuwa ni pamoja na mshindi wa kwanza atakaeibuka na kitita cha shilingi Milioni 2, Mshindi wa pili shilingi milioni 1 na mshindi wa tatu akiibuka na shilingi Laki 5 ambapo zawadi ya mfungaji bora ikiwa ni shilingi Laki moja inayotolewa na Bomba fm redio.

Alisema timu hizo zitacheza kwa mtindo wa ligi ambapo timu zitagawanywa kwenye makundi manne yenye timu tano kila kundi na kisha kupata timu mbili zitakazoingia katika hatua za Nusu fainali, robo na hatimaye fainali.

Alisema kabla ya kuanza kutimua vumbi katika ligi hiyo itatanguliwa na mtanange mkali wa ngao ya Hisani kati ya timu ya Zaragoza fc na Ilemi ambazo zilikuwa kwenye nafasi za juu msimu uliopita.

Alizitaja timu hizo kuwa kundi A,Vijana,Sido Junior,Kabwe United, Pamba nyepesi na FC Leopard, kundi B linaundwa na timu za Cocacola, Airport Rangers, Majiko fc, Sidon a Ilemi, Kundi C lina timu za Wakongwe, Terminal, Wateule, Moning Star na Zaragoza huku kundi la Nne likiwa na timu za Mbaspo, Two in One, Kibogozo, Felali na Chuma chakavu.

Kwa upande wake Meneja usambazaji wa Kampuni ya Cocacola kanda ya Nyanda za juu kusini, Emmanuel Mnyoga, alisema wanajisikia fahari kusaidia kuinua vipaji vya michezo kuanzia ngazi za chini kupitia udhamini wanaoutoa.

Alisema kutoa udhamini kwenye michezo ni sehemu moja wapo ya kurudisha fadhila kwa wateja wao na kutoa mchango katika jamii inayoizunguka kutokana na vipaji vianavyoibuliwa hutokea katika familia za kawaida.

Mwisho.
Na Mbeya yetu

No comments: