Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, May 11, 2014

LIGI YA MPIRA WA MIGUU KOMBE LA BODA BODA KUANZA KUTIMKA JUNI 14

Meneja wa Matukio wa kampuni ya Citysign Promotion & Marketing agency, Geophrey Mwangunguru, ambao ndiyo wandaaji wa ligi hiyo alisema mbali na mwingiliano wa ratiba pia ni maombi ya mdhamini mkuu.

Meneja masoko na mauzo wa Cocacola Mbeya, Jayant Vekaria alisema wanajisikia faraja kutoa udhamini kwa kundi maalumu kama madetreva wa bodaboda ambayo wamekuwa wakisemwa vibaya mitaani.

 Moja ya wadhamini ligi hiyo Nwaka Mwakisu  amesema ndoto yake kubwa katika maisha ni kuona vijana hawakosi kazi ya kufanya na ndiyo maana ameamua kuungana na vijana wenzake kushiriki katika mashindano hayo



Meneja wa Kihumbe, Ptolemy Samwel, ni moja ya wadhamini wa ligi hiyo akiongea na viongozi wa Bodaboda

Meneja masoko na mauzo wa Cocacola Mbeya, Jayant Vekaria akikabidhi jezi kwa moja ya viongozi wa timu ya bodaboda

Moja ya wadhamini ligi hiyo Nwaka Mwakisu akimkabidhi mipira msimamizi wa ligi hiyo

Meneja wa Kihumbe, Ptolemy Samwel, akikabidhi jezi kwa viongozi wa bodaboda










LIGI ya mpira wa miguu ya Kombe la Boda boda 2014 lililokuwa linatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 10, Mwaka huu limesogezwa mbele hadi Juni 14, Mwaka huu kutokana na mwingiliano wa ratiba na ligi zingine.


Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye viwanja vya City Pub jijini Mbeya, Meneja wa Matukio wa kampuni ya Citysign Promotion & Marketing agency, Geophrey Mwangunguru, ambao ndiyo wandaaji wa ligi hiyo alisema mbali na mwingiliano wa ratiba pia ni maombi ya mdhamini mkuu.


Mwangunguru alisema hivi sasa michuano hiyo imepata mdhamini mkuu ambaye ni kampuni ya vinywaji ya Cocacola kwanza Kanda ya Mbeya hivyo kuomba michuano hiyo kusogeza mbele kutokana na kuwepo kwa ligi nyingine ya Mastala cup ambayo inaanza Mei 10, Mwaka huu na kudhaminiwa na Cocacola.

Alisema mdhamini ameona ni vema ligi hizo zikapishana ili kuleta mvuto kwa jamii na kutoa burudani mfululizo kwa wapenzi wa mpira wa miguu katika Jiji la Mbeya kwa kutofautisha ratiba.


Kwa upande wake Meneja masoko na mauzo wa Cocacola Mbeya, Jayant Vekaria alisema wanajisikia faraja kutoa udhamini kwa kundi maalumu kama madetreva wa bodaboda ambayo wamekuwa wakisemwa vibaya mitaani.

Alisema jamii inapaswa kuelewa kuwa madereva wa bodaboda wamejiajiri sawa na ajira zingine hivyo waheshimiwe na kupitia ligi hiyo ndipo jamii itakapowatambua kuwa nao ni raia wema kama walivyo wengine.

Aliongeza kuwa Kampuni yao imeguswa na kundi hilo hivyo kuamua kutoa udhamini mnono unaofikia Shilingi Milioni 14.2  ambazo zitasaidia kuandaa mashindano pamoja na zawadi kwa washindi katika nafasi tofauti tofauti na kwamba ligi hiyo itaitwa Cocacola Bodaboda cup 2014.

Alizitaja zawadi hizo kuwa ni mshindi wa kwanza kujinyakulia Pikipiki mpya moja, mshindi wa Pili fedha taslimu shilingi Laki saba, mshindi wa tatu shilingi laki tatu huku mfungaji bora, timu yenye nidhamu uwanjani na Golikipa bora wakiambulia shilingi laki moja kila mmoja.


Mbali na kuahirishwa kwa ligi hiyo timu zilizothibitisha kushiriki ligi hiyo zilikabidhiwa  vifaa vya michezo ikiwemo mipira na jezi kutoka kwa wadhamini ambao ni kampuni ya Cocacola, Kihumbe na Nwaka Mwakisu ambaye pia ni mlezi wa Chama cha madereva wa bodaboda Mkoa wa Mbeya.

Mwisho.

Na Mbeya yetu

No comments: