Mtendaji wa
Kijiji cha Iwiji Kata ya Iwiji Wilaya ya Mbeya Mkoani Mbeya Anthon Ndisa
anashikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusiana na upotevu wa Mbolea za ruzuku mifuko
189 kwa kipindi cha mwaka 2013/2014.
Kamanda wa
Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amethibitisha kupokea malalamiko kutoka kwa
wananchi wa Iwiji na kumtuma Mkuu wa Polisi wilaya ya Mbeya Richard Mchomvu ili
kujua hatma ya suala hilo.
Katika
mkutano wa hadhara uliofanyika Kijijini hapo na kuhudhuriwa na Afisa tarafa
Sote ambapo Afisa Kilimo Maserlin Mlelwa alitoa takwimu za mgao wa mbolea kwa
kijiji hicho na utaratibu uliotakiwa kufuatwa kugawa mifuko hiyo 189.
Ndisa
alipotakiwa kujieleza katika mkutano huo amedai kuwa alilazimika kuwatumia
wenyeviti wa vitongoji kutokana na kamati ya mbolea ya kijiji kuvunjwa na
wananchi hao jambo ambalo wananchi walilipinga.
Mbolea hiyo
imetolewa na Serikali Mwishonni mwa mwaka jana lakini imedaiwa mbolea hiyo
haikuwafikia walengwa na kuleta malalamiko kijijini lawama kubwa ikielekezwa
kwa mtendaji wa kijiji Anthon Ndisa aliyepewa dhamana ya kusimamia ugawaji wa
pembejeo hizo.
Kwa upande
wake Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mbeya Richard Mchovu amesema kuna taratibu za
kiutawala zilikiukwa hivyo watafungua jalada la uchunguzi kwa mtendaji wa
kijiji hicho na kumpatia mwajiri wake ambaye ni Mkurugenzi wa Wilaya na
ikithibitika hatua za kinidhamu zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kufikishwa
mahakamani.
Mkutano huo
pia ulimtupia lawama Diwani wa Kata hiyo Anderson Kabenga ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kwa kufumbia macho kero za wananchi
licha ya kupewa taarifa mara kwa mara.
Aidha
wananchi hao walikerwa na kitendo cha mtendaji kuwakamata wananchi waliokuwa
wakifuatilia mgao wa mbolea kwa madai ya kumtishia kuuawa tukio lililofanyika
Mwezi Februari mwaka huu na kwenda Polisi Kituo cha Ileje badala ya Mbeya.
Na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment