Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, April 9, 2014

KIPIMO CHA HARAKA CHA MALARIA(mRDT) KATIKA VITUO BINAFSI VYA AFYA MKOANI MBEYA CHAZINDULIWA


Mgeni rasmi kaimu katibu tawala wa mkoa wa Mbeya Nicolaus Ntangu akizindua kipimo cha haraka cha Malaria (mRDT)kwa vituo binafsi vya Afya mkoani Mbeya . 
Amesema Katika hatua ya awali ya utekelezaji wa mradi huu mikoa ya Mbeya, Morogoro na Tanga imechaguliwa kwa ajili ya majaribio. Jumla ya vituo 51 vya binafsi vinavyotoa huduma ya afya kwa mama na mtoto vitahusika katika zoezi hili. Kwa mkoa wa Mbeya Jumla ya vituo 17 vitahusika katika huduma hii ya mRDT. 

Mganga mkuu wa mkoa wa Mbeya  Dk Seif Mhina akimkaribisha mgeni rasmi

Mratibu (PSI) kanda ya nyanda za juu kusini Elia J. Ndutila akitoa taarifa fupi kwa mgeni rasmi amesema watu 30,000 na 60,000 hufa kwaMalaria kwa mwaka na kundi kubwa linalo adhirika ni watoto waliochini ya umri wa miaka mitano na kina mama wajawazito. 

Mratibu Malaria mkoa wa Mbeya Salehe Mwango akisoma taarifa fupi kwa mgeni rasmi


Wamiliki na wahudumu wa vituo vy afya vya binafsi wakiwa makini kumsikiliza mgeni rasmi katika uzinduzi huoNassoro  s  Mohamed  Mtaalamu wa Afya PSI  Kanda ya nyanda za juu kusini akifafanua jambo kwa wamiliki wa vituo binafsi vya afya katika uzinduzi huo
kipimo cha haraka cha malaria-mRDT 


Picha ya pamoja


Na Mbeya yetu

No comments: