Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, April 1, 2014

MBEYA YETU YAPOKEA MSAADA WA MAFUTA KWA WALEMAVU WA NGOZI (ALBINO

Meneja masoko wa asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya nchini Czech ya Bez Mamy, Chris Lameck, akimkabidhi mafuta Jenga James Ambaye ni mlemavu wa ngozi 

Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu akimkabidhi Jenga James mafuta ya kutibu ngozi



Jenga Jemsi(36) mkazi wa Songwe wilayani Mbeya alisema tangu amezaliwa hajawahi kupewa msaada wa mafuta licha ya kusikia kuwepo kwa mafuta mengi kwenye uongozi wa chama chao unaotolewa na watu mbali mbali.





Wananchi mbali mbali wa Nchi ya Jamhuri ya Czech barani Ulaya wametoa msaada wa mafuta ya kutibu ngozi kwa ajili ya watu wenye matatizo hayo(Albino) wa Mkoa wa Mbeya.

Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo kwa mmiliki wa Mtandao wa Mbeya yetu, Meneja masoko wa asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya nchini Czech ya Bez Mamy, Chris Lameck, katika hafla iliyofanyika katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe, alisema msaada huo umetolewa na wananchi na kuuwasilisha kwenye  Asasi hiyo.

Alisema msaada huo hutokana na maombi ya wahusika kutaka kusaidiwa baadhi ya vitu ambapo asasi hiyo hutangaza kwa wananchi ambao hujitolea kadiri wanavyoguswa na asasi hiyo huvituma kwa wahusika ambapo Mkoa wa Mbeya dawa hizo zimekabidhiwa kwenye ofisi za mtandao wa www.mbeyayetu.blogspot.com kwa ajili ya kuwafikishia wenye matatizo ya ngozi.

Mafuta yaliyokabidhiwa ni chupa kumi kwa ajili ya watoto wadogo pamoja na chupa mbili kwa ajili ya watu wazima ambazo alipewa Albino mmoja aliyejitokeza uwanja wa ndege kutokanana kuwa na mahitaji makubwa baada ya ngozi yake kuharibika.

Akishukuru kwa msaada huo Jenga Jemsi(36) mkazi wa Songwe wilayani Mbeya alisema tangu amezaliwa hajawahi kupewa msaada wa mafuta licha ya kusikia kuwepo kwa mafuta mengi kwenye uongozi wa chama chao unaotolewa na watu mbali mbali.

Kwa upande wake moja ya  Wakurugenzi wa Mbeya yetu, Joseph Mwaisango ametoa wito kwa wazazi wenye watoto walio na ulemavu wa ngozi kufika ofisini kwake kuchukua mafuta hayo kwa kuwa ni machache kutokana na kuuzwa gharama kubwa. 

Mafuta hayo tunatoa bure.

Mwisho.

Na Mbeya yetu



No comments: