Vurugu kubwa zimetokea mkoani Mbeya
baina ya Jeshi la Polisi na waendesha bodaboda(pikipiki) baada ya jeshi la
polisi kutaka kuzima jaribio la kutaka kuvunja nyumba.
Boda boda hao walifunga barabara na
kuzua taflani baina yao na jeshi la Polisi baada ya Jeshi hilo kuingilia kati
kumuokoa Mke wa dereva wa pikipiki baada ya madereva hao kuvamia nyumba yake
maeneo ya Forest wakitaka kubomoa wakimtuhumu kuhusika na kifo cha mumewe.
Tukio hilo limetokea leo majira ya saa
nne asubuhi baada ya waendesha bodaboda kutaka kumdhuru mwanamke huyo
wakimtuhumu kumuua dereva mwenzao ndipo jeshi la polisi lilipoingilia kati
hivyo kusababisha vurugu kubwa baina ya madereva hao na jeshi la polisi.
Hata hivyo madereva wa pikipiki zaidi ya
20 walilivamia gari la Polisi na kuvunja kioo cha mbele hali iliyopelekea
dereva wa gari hilo kulikimbiza hadi kituo cha Polisi cha Kati ili kuomba
msaada kwa askari wenzie waliojitokeza wakiwa na silaha za moto na kuwatawanya
kabla ya kufunga barabara na kuanzisha vurugu.
Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha
bodaboda Jiji la Mbeya, Vicent Mwashoma, amelaani kitendo hicho na kuongeza
kuwa jeshi la polisi limetumia nguvu kubwa kupambana na madereva wa bodaboda
ili hali kuna uongozi unaotambuliwa na kusimamiwa na baadhi ya Askari.
Akizungumzia chanzo cha vurugu hizo,
mwenyekiti huyo amesema juzi aliuawa dereva mwenzao aliyemtaja kwa jina la Siza
Mwambenja ambapo baada ya kuzika madereva hao walianza kufanya upelelezi na
kupewa taarifa kuwa aliyehusika ni mkewe aliyeachana naye kwa kusuka njama na
wauaji.
Amesema baada ya kupata taarifa hiyo
walienda nyumbani kwake kwa lengo la kumkamata hali iliyosababisha jeshi la
polisi kufika na kuwatawanya lakini jazba ziliwapanda madereva hao baada ya
baadhi ya maaskari kuanza kuvunja pikipiki na kuwapiga.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo
wamesema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi baada ya marehemu kuachana
na mke wake huyo anayetuhumiwa kusuka njama za mauaji na kuoa mke mwingine hali
iliyosababisha mwanamke huyo kupata wivu na kulazimika kufanya mipango ya
mauaji hayo.
Wakati vurugu hizo zikiendelea Shule ya
sekondari ya Forest ya Jiji la Mbeya ililazimika kuahirisha mitihani ya
kufungia mhula kutokana na wanafunzi kuathirika na mabomu yaliyokuwa yakirushwa
na jeshi la polisi.
Hata hivyo kufuatia vurugu hizo
waendesha boda boda kadhaa wanashikiliwa na jeshi la polisi akiwemo Katibu wa
chama hicho kwa kuhusika na uvunjaji wa Sheria na uharibifu wa miundombinu ya
barabara na gari la Polisi.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
2 comments:
Kwanza nianze kwa kutoa pole sana kwa wale wote walio husika kwenye tukio hili, lakini pia nitoe ushauri wangu kwa pande zote mbili nikimaanisha serikali pamoja na vijana hao waendesha bodaboda. kwamba kila taifa lina sheria zake, ambazo zinalifanya taifa hilo kuendesha vizuri nchi husika. kwaiyo ni vyema kwa pande zote mbili kulinda na kuheshimu sheria za nchi, japo kuna watakao sema wao ndio wameonewa lakini ni vyema sheria zikachukua mkondo wake juu ya tukio hili.
http:mutalemwa-masgider.blogspot.com
Hivi nchi yetu inapelekwa wapi na umoja za kipumbavu kama bodaboda; ukawa; uhamsho; n.k mi nadhani hata nguvu iliyotumika polisi ni ndogo waache upumbavu wao.
Post a Comment