Hii ndio Hali halisi ya Barabara ya Block T ambapo imeharibika na kusababisha Dala dala kutaka kugomea kupita katika Eneo hilo kuhofia kukwama.
Hii ni sinto Fahamu ambapo wakati waandishi wa Habari waliojitolea kurekebisha Barabara hiyo wakiendelea na kazi ya kuziba mashimo hayo , watumishi wa Jiji wenyewe walikuwa ndani ya Gari lao wamefunga vioo na kushangaa kinacho endelea bila kuonesha ushirikiano wowote na Baadae waliondoka, Jambo ambalo limewashangaza watu wengi, Huku wakiwa wameahidi wangerekebisha Muundombinu huo.
Mmoja ya Gari dogo likiwa limesimama baada ya kuona kuwa Njia ni mbaya
Baadhi ya Waandishi wa Habari Kutoka Bomba Fm wakishirikiana na Mbeya yetu Blog wakianza kuchukua Kifusi na Kuziba Barabara hiyo.
Msimamizi Mkuu na Mwandishi wa Mbeya yetu Blog Joseph Mwaisango akiwa anaendelea na kazi ya kuziba eneo hilo lililoharibika
Hali halisi ya Njia hiyo
Mmoja wa wasukuma Mkokoteni akiwa amejitosa kupita katika tope na kuendelea na safari , kutokana na kwamba alikuwa hana Njia nyengine zaidi ya hiyo
Baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka Bomba Fm Radio wakiendelea na Kazi
Kazi imepamba moto ambapo waandishi wa Habari kutoka Bomba FM wakiwa wamekomaa kuendelea kuziba mashimo katika barabara hiyo iliyo haribika kwa kiwango kikubwa huku wakazi na wafanya biashara wa eneo hilo wakiwa wanatazama bila kufanya juhudi zozote za kutengeneza, lakini wakisikia kuna mgomo wanakuwa wakwanza kwenda andamana na shughuli za kijamii kama hizi kuzisusia
Kazi ikiwa inaendelea kwa kasi ili kupisha Magari yaanze kutumia Njia hiyo huku Wakazi na wafanyabiashara wa eneo hilo wakiwa wanapaangalia tu, na Jiji kufika hapo na gari lao bila kufanya kitu chochote
Kazi ikiwa inaendelea kwa kasi kubwa
Kila mmoja yupo bize
Kazi inaendelea kusonga mbele
Picha na Mbeya yetu
Picha na Mbeya yetu
********************************
Mbeya yetu Blog kwa ushirikiano mkubwa kabisa na Bomba Fm Radio (elimisha burudisha) waamua kurekebisha kipande cha barabara inayo tumika
kupitia daladala zinazo toka uyole kuelekea s/kuu kipande hicho kilichopo Block
'T'
Ushirikiano huo wa
vyombo hivyo viwili vya habari umekuja baada ya madereva wa daladala kutaka
kuweka mgomo kwaajiri ya kipande hicho cha barabara kuwa kibovu kinachokuwa ni tatizo kwa daladala hizo.
Bomba Fm Radio na mbeya yetu Blog wamechukua hatua hiyo ili
kuepusha migomo isiyo kuwa yalazima kutokana na kupenda amani na kuwajali
watanzania ambapo Halimashauri ya Jiji ilitoa ahadi ya kutengeneza lakini mpaka
sasa haijaweza kufanya jambo lolote kuhusiana na sehemu hiyo.
Mtazamo : Halimashauri
ya Jiji la Mbeya mnapo wahamisha watu kutoka sehemu moja kuelekea sehemu
nyingine tunaomba muhakikishe mmewawekea miundombinu ya kutosha ili kuepusha
mambo machache yanayo weza kuwa ni tatizo kwa wananchi
No comments:
Post a Comment