Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, April 17, 2014

KIKOSI CHA MABORESHO YA TAIFA STARS CHA TAJWA.

Kocha Msaidizi, Salum Mayanga, aliyekuwa na timu hiyo katika Mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hill View iliyopo jijini Mbeya.


Katibu  wa chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA) Selemani Harubu


Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya 






Add caption



HATIMAYE Wachezaji 16 wa kikosi cha Maboresho ya Timu ya Taifa(Taifa stars) kimechaguliwa kutoka kwenye kambi iliyokuwa ikifanyika katika Uwanja wa Chuo cha Ualimu Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya iliyokuwa na wachezaji 34.

Kikosi hicho  kimetangazwa leo na Kocha Msaidizi, Salum Mayanga, aliyekuwa na timu hiyo katika Mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hill View iliyopo jijini Mbeya.

Mayanga aliwataja wachezaji hao kuwa ni Mlinda mlango Benedict Tinoko Mlekwa kutoka Mara, Walinzi wa kati ni Emma Namwondo Simwanda kutoka Temeke na Joram Nason Mgeveja kutoka Iringa.

Aliwataja walinzi wa pembeni kuwa ni Omari Ally Kindamba kutoka Temeke, Edward Peter Mayunga kutoka Kaskazini Pemba na Shirazy Abdallah Sozigwa kutoka Ilala,viongo wa Ulinzi ni Yusufu Suleiman Mlipili na Said Juma Ally kutoka Mjini Magharibi.

Viongo Washambuliaji ni Abubakar Ally Mohamed kutoka Kusini Unguja na Hashimu Ramadhani Magona kutoka Shinyanga, na Viungo wa pembeni ni Omari Athumani Nyenje kutoka Mtwara na Chunga Said Zito kutoka Manyara.

Aliwataja washambuliaji kuwa ni pamoja na Mohammed Seif Said kutoka Kusini Pemba, Ayubu Kassim Lipati kutoka Ilala, Abdurahman Othman Ally kutoka Mjini Magharibi na Paul Michael Bundara kutoka Ilala.

Aliongeza kuwa katika kikosi hicho pia wamechaguliwa wachezaji wawili waliojiunga na Timu ya Taifa ya wenye umri chini ya Miaka 20 ambao ni Mbwana Mshindo Musa kutoka Tanga na Bayaga Atanas Fabian kutoka Mbeya.

Aidha Kocha huyo alisema wachezaji wengine walioachwa wataendelea kuwa kwenye uangalizi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF) kwa sababu mpango wa maboresho ya timu ya Taifa ni endelevu.

Alisema Kambi ya timu hiyo ilianza Machi 22, Mwaka huu na kuhitimishwa Aprili 17, mwaka huu kwa awamu ya kwanza ambapo wachezaji hao watajiunga na kikosi cha Timu ya Taifa cha Awali kwa ajili ya maezo ya mechi ya Kirafiki kisha watarudi tena wilayani Rungwe kwa ajili ya Kambi ya awamu ya Pili.

Mwisho.

Na Mbeya yetu

No comments: