Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia Jiji la Mbeya Lucas Mwampiki
Katibu
Mwenezi wa Chama cha Demokrasia Jiji la Mbeya Lucas Mwampiki amejiuzuru wadhifa
huo kuanzia Aprili mwaka huu kutokana na mkanganyiko wa uongozi ndani ya chama
hicho.
Mwapiki
amesema amechoshwa na marumbano ya mara kwa mara na meza kuu ndani ya chama hicho
katika ngazi ya wilaya hivyo kudhoofisha juhudi zake za kukijenga chama hicho.
Aidha
Mwampiki amesema viongozi wa chama hicho wamekuwa na marumbano ya mara kwa mara
hivyo yeye kama kiongozi hayupo tayari kuona mambo yanavurugika katika chama
hicho.
Hata hivyo
katika uamuzi aliouchukua Lucas Mwapiki amesema kuwa yeye atabakia kuwa
mwanachama wa chama hicho na Diwani wa Kata ya Mwakibete Jijini Mbeya.
Amewataka
wanachama wamuelewe hivyo ameona yeye akae pembeni badala ya kuwa na muda
mwingi wa kujadili migogoro ambayo haina tija na kuleta mkanganyiko kwa
wanachama.
Na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment