HALMASHAURI ya Busokelo katika Wilaya ya Rungwe na Shirika
la nyumba (NHC) wameingia kwenye makubaliano ya msingi ya kujenga nyumba 14 kwa
ajili ya watumishi wake.
Uamuzi wa kujenga nyumba hizo unalenga kuboresha utendaji na ufanisi wa halmashauri
hiyo mpya iliyoanzishwa 2012, huku
ikiwa inakabiliwa na tatizo kubwa la miundombinu, ikiwemo nyumba za watumishi.
Akizungumza na waandhishi wa habari Jijini hapa, ikiwa
ni muda mfupi baada ya kumalizika kikao cha pamoja na watendaji wa shirika la
nyumba, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Meckson Mwakipunda, alisema mpango huo
wa ujenzi wa makazi ya watendaji ni sehemu ya miradi ya kipaombele katika
halmashauri hiyo.
“Kama mnavyojua Busokelo ni halmashuri mpya ambayo ilianza
rasmi Oktoba 10 mwaka 2012, na upya huo inachangamoto nyingi hasa makazi ya
watumishi na kwenye bajeti yetu ya kwanza ambayo ndio tunaendelea nayo
tuliingiza hilo la kujenga nyumba lengo likiwa ni kuwajali wafanyakazi kwa kuwapa mazi bora ” .
Alisema halmashauri hiyo ilitenga kiasi cha shilingi milioni
500 kwa ajili ya mradi wa kuboresha makazi, ambao umegawanyika katika awamu
mbili, awamu ya kwanza ikiwa ni kujenga nyumba 14 za watumishi, huku awamu ya
pili ikihusisha nyumba 36 kati ya 50 zitakazuhusisha miradi hiyo, ambapo baadhi ya nyumba hizo
zitauzwa na kupangishwa kwa wananchi wa kawaida.
Alisema serikali kwa kutambua changamoto ilikubali kuthibitisha bajeti hizo na
tayari fedha hizo zimeshaingizwa katika halmashauri hiyo na kilichobaki ni
kukamisha hatua za kisheria kati yake na mkandarasi ambaye ni shirika la nyumba
ambalo litahusika katika ujenzi huo.
Akizungumzia muda wa kuanza kwa mradi huo, Mwakipunda
alisema kinachosubiliwa hivi sasa ni halmashauri hiyo kupata Baraka za Wizara
ya Tawala za Mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi) ambayo ndiyo yenye mamlaka
ya kuidhinisha vibali vya miradi ya aina hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la nyumba, Martin Mdoe,
alisema mradi wa makazi Busokelo ni sehemu ya mkakati wa miaka mitano wa
shirika hilo kujenga nyumba za gharama nafuu za madaraja tofauti touti katika
maeneo mbalimbali nchini, zikiwemo halmashauri.
“Kipaumbele cha mkakati huu ni kwa halmashauri mpya 16
nchini, ambazo katika maeneo yao hakuna nyumba za kutosha , miongoni mwa
halmashauri hizo katika mkoa wa Mbeya tumeanza na Halmashauri ya Busokelo”
Mwisho.
Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment