Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, March 4, 2014

VYOMBO VYA HABARI NDIYO KICHOCHEO KIKUBWA CHA AMANI DUNIANI



 Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk Norman Sigalla King ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro katika hafla ya kufungua mafunzo ya kituo cha Redio cha Bomba kilichopo Jijini Mbeya yanayotolewa na Shirika la Utangazaji la BBC.

Mwezeshaji wa mafunzo kutoka Shirika la Utangazaji la BBC la Uingereza, Pendael Omary, alisema lengo la mafunzo hayo ni kuongeza weledi wa kazi ya habari kwa vituo vya Redio vya Mikoani.

Meneja wa kituo cha Radio Bomba FM Fredy akifafanua jambo katika mafunzo hayo











VYOMBO vya habari vimeelezwa kuwa ndiyo kichocheo kikubwa cha amani duniani kote hivyo vinapaswa kutoa taarifa zenye kuhamasisha hali ya amani na utulivu katika jamii ya Tanzania.

Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk Norman Sigalla King ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro katika hafla ya kufungua mafunzo ya kituo cha Redio cha Bomba kilichopo Jijini Mbeya yanayotolewa na Shirika la Utangazaji la BBC.

Alisema kujengeka au kutokujenga kwa amani katika jamii kunategemea vyombo vya habari jinsi vilivyotangazana hivyo Wananchi kuhamasika  kutokana na kile wanachokisikia na kuelezwa.

Kwa upande wake Mwezeshaji wa mafunzo kutoka Shirika la Utangazaji la BBC la Uingereza, Pendael Omary, alisema lengo la mafunzo hayo ni kuongeza weledi wa kazi ya habari kwa vituo vua Redio vya Mikoani.

Alisema vyombo vya habari vinakazi ya kubadilisha maisha ya watu kupitia vipindi mbali mbali vinavyotangazwa ambavyo vinakuwa vimefanyiwa utafiti na kuwa na manufaa kwa jamii.

Na Mbeya yetu

No comments: