Meya wa Jiji
la Mbeya Athanas Kapunga ameishukuru Serikali kwa kuiwezesha Hospitali ya Rufaa
Mbeya kupata vifaa vya kupimia magonjwa ya figo.
Kauli hiyo
ameitoa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya katika maadhimisho ya siku ya figo
nchini ambapo wakazi wa Mbeya wamejitokeza kupima ili kujua Afya zao na
maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Daktari Onesmo Kisanga kutoka Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili.
Kisanga
ambaye ni Rais wa Madaktari wa figo nchini amesema hivi sasa kumekuwa na
ongezeko la wagonjwa wa figo kila siku hiyo inatokana na wananchi wengi
kutopima afya zao hali ambayo ingeweza kuzuia matatizo makubwa ambayo hupelekea
gharama kubwa za upasuaji.
Aidha
Daktari bingwa amesema pia uhaba wa Madktari wa fani hiyo unawafanya waliopo
kupata msongamano mkubwa wa wagonjwa kutoka mikoani pia wengi kofahamu kuwa
hivi sasa Serikali imesogeza huduma hiyo katika Hospitali za Rufaa ikiwemo
Mbeya yenye madaktari watatu wa figo.
Kati ya
Madaktari watatu wawili ni raia wa Cuba na mmoja ni Mzalendo anayefahamika kwa
jina la Octabenny Kassanga ambaye amewataka wananchi wa Mbeya kufika Hospitali
ili waweze kujua Afya zao na kupatiwa tiba sahihi na ushauri ili kudhibiti
ongezeko la ugonjwa huo ambao ukicheleweshwa gharama zake ni kubwa ambazo na
zaidi ya shilingi milioni ishirini.
Kaimu
kurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Daktari Omari Salehe amewataka wananchi
kujitokeza kwa wingi katika Hospitali ya Rufaa ili kuokoa gharama kwani wanazo
mashine za kisasa pia mdaktari waliobobea katika fani ya magonjwa ya figo
ambapo katika siku mbili wagonjwa watapatiwa huduma ya vipimo bure kuanzia
Machi 12 hadi Machi 14 mwaka huu.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment