Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, March 13, 2014

MRADI MPYA WA KIHUMBE WA KITUO CHA KUKUZA UJUZI KWA VITENDO WAZINDULIWA MBEYA

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Norman Sigala alipokuwa anazindua mpango wa kuwajengea uwezo wanafunzi 60 waliomaliza mafunzo ya ushonaji na ufundi magari baada ya kupata msaada wa vifaa vipya vya kisasa kutoka shirika la IMARISHA la Marekani.

Mkurugenzi wa mradi wa IMARISHA Nchini Bi Colleen Green amesema analipongeza shirika la KIHUMBE kwa mpango madhubuti wa kuwajengea maarifa vijana wanaoishi katika mazingira hatarishi hivyo wao wataendelea kutoa msaada wa vifaa ili kuwafanya waweze kujiajiri au kuajiriwa ambapo wataondokana na wimbi la ukosefu wa ajira nchini.

Bi Joan Mayer Mratibu kutoka Shirika la USAID anayesimamia mikoa ya Iringa na Njombe amesema kuwa mpango wa kuwajengea uwezo vijana hao utawafanya vijana hao kumaliza mafunzo wakiwa na mitaji yao hali itakayowafanya kumaliza mafunzo wakiwa wameimarika kiuchumi na kuwa na ufanisi mkubwa wa taaluma ya ufundi.


 Mkurugenzi wa Mradi wa Imarisha na Kihumbe, Ptolemy Mwakanyamale akisoma taarifa fupi mbele ya mgeni rasmi 

Baadhi ya wahitimu wakiwa katika uzinduzi huo

Baadhi ya wawakilishi kutoka shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani


Wadau mbali mbali walihudhuria tukio hilo la uzinduziWageni waalikwa

Mshereheshaji

Manuku Mkurugenzi katika moja ya gereji maeneo ya soweto akifafanua jambo jinsi wanavyoshirikiana na KIHUMBE

Moja ya wahitimu  ufundi magari akitoa shukrani zake  za kuhitimu mafunzo


Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Norman Sigala akiangalia jinsi wahitimu wa ufundi makenika wakinyanyua gari kwa mtambo maalum

Mkurugenzi wa mradi wa IMARISHA Nchini Bi Colleen Green akimwangali moja ya wahitimu akishona nguo

Mkurugenzi wa mradi wa IMARISHA Nchini Bi Colleen Green akipata maelezo mafupi toka wahitimu

Serikali imezitaka Asasi zinazoshughulika na Vijana wanaoshi katika mazingira magumu na hatarishi kuwajengea uwezo wa kujiajiri na kuajiriwa.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro katika shirika la KIHUMBE ambapo aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Norman Sigala alipokuwa anazindua mpango wa kuwajengea uwezo wanafunzi 60 waliomaliza mafunzo ya ushonaji na ufundi magari baada ya kupata msaada wa vifaa vipya vya kisasa kutoka shirika la IMARISHA la Marekani.

Mkurugenzi wa KIHUMBE Ptollemy Mwakanyamale amesema kuwa Asasi yao imekuwa ikitoa mafunzo ya ufundi lakini wahitimu wake wamekuwa wakikabiliwa na ukosefu wa ajira kutokana na kukosa vifaa vya kufanyia kazi na mbinu za kisasa za kukabiliana na soko la ajira.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa mradi wa IMARISHA Nchini Bi Colleen Green amesema analipongeza shirika la KIHUMBE kwa mpango madhubuti wa kuwajengea maarifa vijana wanaoishi katika mazingira hatarishi hivyo wao wataendelea kutoa msaada wa vifaa ili kuwafanya waweze kujiajiri au kuajiriwa ambapo wataondokana na wimbi la ukosefu wa ajira nchini.

Aidha Bi Joan Mayer Mratibu kutoka Shirika la USAID anayesimamia mikoa ya Iringa na Njombe amesema kuwa mpango wa kuwajengea uwezo vijana hao utawafanya vijana hao kumaliza mafunzo wakiwa na mitaji yao hali itakayowafanya kumaliza mafunzo wakiwa wameimarika kiuchumi na kuwa na ufanisi mkubwa wa taaluma ya ufundi.

Mkuu wa Mkoa amesema Asasi za aina hiyo zinasaidia kuondoa vitendo vya kihalifu lakini pia kuimarisha mapambano dhidi ya Ukimwi ambapo vijana wengi wamekuwa wakiathiriwa zaidi kutokana na ukosefu wa ajira.

Kandoro amesema kuwa elimu ya ufundi inawapa wahitimu uwezo wa kuajiri hata watu waliomaliza ngazi ya vyuo vikuu na wao watakua waajiri kutokana na kumaliza wakiwa na ujuzi na mitaji yao kutokana na mbinu bora zilizobuniwa ili kukabiliana na wimbi la vijana ambao wengi wamekuwa wakimaliza mafunzo ya ufundi lakini wamekuwa wakikosa ajira.

Na Mbeya yetu

No comments: