Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, March 13, 2014

UKATILI DHIDI YA WATOTO BADO NI TISHIO MBEYA

John Msumba[3]ambaye amekuwa akipigwa mara kwa mara na wakati wote kufungiwa ndani kwa kufuli pia kunyimwa chakula na shangazi yake 


TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HII KWANI HATUNA JINSI IMEBIDI TUONYESHE  KILA SEHEMU YA MWILI YA MTOTO HUYU KWA MATESO ALIYOKUWA AKIPATA HATA KUKAA ANASHINDWA

Shangazi huyu ndiye anaetuhumiwa kumtesa mtoto huyu


 Mwanahawa Nassoro[32] mkazi wa mtaa wa Airport Kata ya Iyela. ndiye anaetuhumiwa kumtesa  mtoto John Msumba

Hali ya kiafya ya mtoto huyo si nzuri

Vidole vimevimba kutokana na vipigo vya mara kwa mara

Jeraha kubwa juu ya jicho la mtoto huyo kutokana na kipigo toka kwa shangazi yake

Hiki ndicho chumba alichokuwa anafungiwa mtoto huyo



Licha ya Asasi mbalimbali za kijamii kama TAMWA, GBV,TGNP na Dawati la jinsia la Jeshi la Polisi kukemea vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto Mkoani Mbeya bado vitendo hivyo vimeendelea kushamiri.

Katika matukio mawili yaliyotokea Jijini Mbeya hivi karibuni yamewakumba watoto wawili wa wakazi wa Kata za Iyela na Iduda ambao wamejeruhiwa vibaya kwa vipigo na kuchomwa moto na walezi wao.

Tukio la kwanza limemhusisha mtoto wa kiume aliyefahamika kwa jina la John Msumba[3]ambaye amekuwa akipigwa mara kwa mara na wakati wote kufungiwa ndani kwa kufuli pia kunyimwa chakula na shangazi yake aitwaye Mwanahawa Nassoro[32] mkazi wa mtaa wa Airport Kata ya Iyela.

Vitendo hivyo vimetokana na kudaiwa mtoto huyo kujisaidia hovyo hali iliyomletea usumbufu Mwanahawa ambapo mama yake hayupo na Baba mzazi aliyefahamika kwa jina la Sumba Dinda akiwa machimboni wilaya ya Chunya takribani miezi miwili iliyopita.

Sakata hilo lilibainika baada ya kutokea msiba mtaani hapo Machi 12 mwaka huu majira ya saa nne asubuhi mtoto huyo alipokuwa akilia majirani walisogea eneo la tukio na kukuta mlango umefungwa kwa kufuli hivyo kumlazimu Mjumbe wa mtaa Bi Rehema Mohammed kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa mtaa huo Enock Mwampagama.

Mwampagama alitoa taarifa kwa Mtendaji wa mtaa Henry Chaula ambapo walimkamata kwa mahojiano katika ofisi ya mtaa na baada ya maelezo walimpeleka kituo cha Polisi Mwanjelwa kwa hatua zaidi.

Uchunguzi umebaini kuwa mtoto huyo amekuwa akiteswa kwa muda mrefu ingawa majirani na mwenye nyumba aliyefahamika kwa jina la Ollen Kaguo hawakuweza kutoa taarifa ili kunusuru afya ya mtoto ambaye ameonekana kuwa na ukosefu wa chakula bora na mwili ukiwa umejaa majeraha makubwa.

TUKIO LA PILI
 Mtoto Anjela Rashid[4]amechomwa moto mikono yote miwili  na baba yake mzazi baada ya kula finyango mbili za nyama zilizopikwa na Baba yake huyo

Inasikitisha sana 

Mtoto amelala bila ya uwangali zi wa mtu yeyote yule



Mtendaji wa mtaa huo Emmanuel Malema akihesabu mabati ili yauwze kwa ajili ya matibabu ya mtoto huyo

Hapa ndipo anapo lala mtoto huyo


Mabati yakitolewa ili yauzwe zipatikane fedha za matibabu ya mtoto huyo


Tukio la  pili limetokea machi 8 mwaka huu mtaa wa Kanda ya juu kata ya Iduda ambapo mtoto Anjela Rashid[4]ameunguzwa na moto mikono yote miwili  baada ya kula finyango mbili za nyama zilizopikwa na Baba yake.

Mama yake mzazi wa mtoto huyo hakuwepo wakati wa tukio hilo kutokana na kukimbia kwa mumewe Rashid Mwatiya[32]  ambapo amekimbilia Sumbawanga Mkoani Rukwa majuma mawili yaliyopita ili kuwepa vipigo vya mara kwa mara alivyokuwa akipata.

Baada ya kutenda unyama huo Mwatiya alimfungia mtoto huyo ndani bila kumpatia matibabu yoyote na chakula kwa hofu ya kukamatwa kutokana na majeraha makubwa mikononi hali inayomfanya mtoto kushindwa kula chakula kwa kutumia mikono.

Kutokana na vidonda kutopatiwa matibabu vidole vimeanza kuoza na kutokana na maumivu makali mtoto amekuwa akilia mara kwa mara ndipo kilio hicho kilibainishwa na Balozi Shaban Tolinga ambaye alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa mtaa lakini hakuchukua hatua zozote huku mikono ya mtoto ikioza.

Hata hivyo Mtendaji wa mtaa huo Emmanuel Malema baada ya kupata taarifa ya ukatili huo aliamua kufuatilia akiwa na waandishi wa habari ambapo mtoto alikuwa amelala sebuleni bila uangalizi wowote na njaa hali ilyomlazimu Mtendaji kuchukua mabati manne kuyauza ili kumpatia matibabu na chakula na kuhakikisha mtuhumiwa anakamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa sheria.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Kata ya Iduda amesema vitendo vya kikatili katika Kata yake vimekuwa vikifumbiwa macho kwa hofu ya kujenga uadui kwa watu wanaotoa ushahidi.

Aidha Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa amesema vitendo vya kiatili havita vumiliwa hivyo wananchi watoe ushirikiano ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo vimekithiri kwa siku za hivi karibuni.

Na Mbeya yetu


2 comments:

Anonymous said...

huu ni unyama kweli kweli! how can you do this to a child! please endelea kutupa habari za mtoto hasa kuhusu matibabu maybe we can help somehow. Toronto

Mwangwitwa Chris said...

Mbeya ni kwetu lakini duuu baadhi ya watu hawana huruma kabisa sasa hawa watoto wana makosa gani mpaka wawaumize hivi? issue ni vinyango vya nyama,ni umaskini wa ajabu sana huu,wazazi tuwe na roho za huruma kwa watoto wetu