Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, March 25, 2014

SEMINA YA MTANDO WA JINSIA(TGNP) KWA WAANDISHI WA HABARI MBEYA

Ofisa wa kitengo cha habari na mawasiliano wa TGNP, Deo Temba.akizungumza katika semina ya kujadili changamoto za jinsia, uchaguzi wa serikali za mitaa na mchakato wa katiba mpya kwa wanahabari.


Waandishi wahabari wakisikiliza kwa makini




Washiriki wa semina hiyo wakifuatilia kwa makini mafunzo yanayofanyika katika ukumbi wa Coffee Garden jijini Mbeya.


WANANCHI wametakiwa kupewa elimu juu ya umuhimu wa uchaguzi wa serikali za mitaa ili kuwawezesha kupata viongozi bora watakao saidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii.

Aidha imeelezwa kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa ni muhimu kuliko uchaguzi mkuu kutokana na kupata viongozi wa ngazi ya chini ya Vitongoji na Vijiji ambako ndiko wananchi wenye hali ngumu wanapatikana hivyo kutokana na elimu itasaidia kupata viongozi bora.

Hayo yamebainishwa  na Afisa Uhusiano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP), Deo Temba katika mafunzo ya wanahabari wa Mkoa wa Mbeya kuhusu namna Waandishi wa habari wanavyochangia kutatua changamoto zinazoikabili jamii, yaliyofanyika katika ukumbi wa Coffee Garden iliyopo jijini hapa.

Alisema Wanahabari wanapaswa kuwa wa kwanza kuelimishwa kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Mwaka huu ili wao wakatoe elimu hiyo kwa wanajamii ili kuona umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi huo kwa manufaa ya maendeleo yao.

Alisema viongozi wa vijiji na vitongoji ndiyo wanaoishi na wananchi kwa ukaribu na kuzijua changamoto mbali mbali zinazoyakabili maeneo husika ambapo wananchi wanapaswa kupewa elimu jinsi ya kupata viongozi watakaowafaa na kusaidia kutatua changamoto zao na siyo bora kiongozi.

Mbali na hayo Afisa huyo aliongeza kuwa  Wajumbe wa bunge maalum la kupitia mchakato wa katiba mpya unaoendelea  mkoani Dodoma wanapaswa kuhakikisha maswala yote yanaigusa jamii yapewe kipaumbele na kutamkwa wazi katika Katiba mpya na siyo kuzungumzia muundo wa Serikali.

Aidha katika mafunzo hayo, Waandishi, na Mtandao wa jinsia(TGNP) walijadili changamoto zinazowakabili katika kuibua maswala ya jinsia katika jamii na namna ya kukabiliana nayo, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na mchakato wa Katiba mpya na umuhimu katika jamii.

Mwisho.

Na Mbeya yetu

No comments: