Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, March 9, 2014

MARY MWANJELWA AWAASA WANAWAKE

Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Mbeya(CCM), Dk. Mary Mwanjelwa wakati akizungumza na wanawake katika kilele cha Siku ya Mwanamke duniani, ambapo alikuwa Mgeni rasmi katika sherehe zilizoandaliwa na Wanawake wa Jiji la Mbeya zilizofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi RuandaNzovwe jijini hapa.



 Rehema ngao, akisoma risala kwa niaba ya wanawake wa Jiji la Mbeya.



  Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, akipokea risala.


Burudani mbalimbali zilikuwepo








Mwanamke Hadhara Njelya mwenye uwezo wa kuchezea mpira jinsi atakavyo 



WANAWAKE WA MUST



WANAWAKE  wameshauri bunge maalumu linaloendelea na Mchakato wa katiba mpya kuhakikisha wanaweka vipengele ambavyo vitamtambua na kumpa haki za Msingi Mwanamke.


Aidha imeelezwa kuwa katika Katiba hiyo pia ikemee mila potofu zinazomdhalilisha mwanamke kama vile ukeketaji na ndoa za umri mdogo pamoja na unyanyasaji wa kijinsia hususani wajane kupokonywa haki za kurithi na kusimamia miradi inayoachwa na mumewe.

Hayo yalitolewa na Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Mbeya(CCM), Dk. Mary Mwanjelwa wakati akizungumza na wanawake katika kilele cha Siku ya Mwanamke duniani, ambapo alikuwa Mgeni rasmi katika sherehe zilizoandaliwa na Wanawake wa Jiji la Mbeya zilizofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi RuandaNzovwe jijini hapa.

Dk. Mwanjelwa alisema endapo haki za Mwanamke zikatambuliwa kikatiba itakuwa njia rahisi kusimamia na kuwachukulia hatua wale wote watakaokiuka na kwenda kinyume.

Aliongeza kuwa Siku ya Wanawake duniani ilitokana na mfumo dume uliosababisha wanawake kudai haki zao bila mafanikio hivyo kupelekea kuwepo kwa siku maalumu ya kukumbushana mambo yanayopaswa kukemewa.

Aidha aliwataka wanawake kuacha kubweteka kutokana na kuwepo kwa vyombo vingi vya kuwatetea bali wafanye kazi kwa bidii ili kutoa nafasi ya kuepuka kuwa ombaomba na kunyanyaswa na waume zao.

Na Mbeya yetu

No comments: