MBEYA
ILI kudhibiti na kuhakikisha Mamlaka ya
maji safi na usafi wa Mazingira Mbeya inakusanya madeni yote kutoka kwa wadaiwa
sugu imeamua kupita nyumba kwa nyumba kwa wateja wenye madeni ili waweze
kulipa.
Hatua hiyo imefanyika kwa Mamlaka ya
maji safi na usafi wa Mazingira Mbeya ikishirikiana na Ofisi za Bonde la
Ziwa Rukwa, katika kuadhimisha kilele cha wiki ya maji zilizoanza Machi 16,
Mwaka huu na kuhitimishwa Machi 22, Mwaka huu kwa mamlaka hiyo kufanya shughuli
za usafi.
Akizungumza katika sherehe za
maadhimisho hayo zilizofanyika katika viwanja vya Ofisi za Mamlaka ya Maji na
usafi wa Mazingira Mbeya, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Simioni
Shauri alisema wiki lote hilo wameshafanya shughuli zaidi ya nne.
Alizitaja shughuli hizo kuwa ni pamoja
na usafi kwenye maeneo yote yenye miundombinu ya mamlaka, kutoa elimu kwa
wateja kuhusu huduma wanayopewa na kuwahimiza kuilipia kikamilifu ambapo
Mamlaka imeamua kupita nyumba kwa nyumba kwa wateja wenye madeni ili waweze
kulipa.
Alisema shughuli zingine ni pamoja na
kutoa elimu kwa wafanyakazi kuhusu namna miundombinu ya maji safi na majitaka
inavyofanya kazi kwa kutembelea miundombinu hiyo pamoja na semina kwa
wafanyakazi na wadau kuhusu Huduma bora kwa mteja na umuhimu wa kulipia maji,
usimamizi wa vyanzo vya maji na udhibiti wa upotevu wa maji.
Kwa upande wake Mgeni rasmi katika
maadhimisho hayo, Idrisa Msuya ambaye ni Afisa maji bonde la Ziwa Rufiji
alisema kauli mbiu ya mwaka huu katika kuadhimisha wiki ya maji ni Uhakika
wa maji na nishati inatokana na upatikanaji wa nishati ya umeme nafuu
kuzalishwa kwa maji.
Alisema maji kwa ajili ya uzalishaji wa
nishati ya umeme hayawezi kupatikana iwapo vyanzo vyake havitatunzwa na
matumizi yake hayaratibiwa vizuri ili kuondoa matumizi mabaya ya maji pamoja na
upotevu.
Alisema uharibifu na matumizi mabaya ya
maji yalisababisha kupungua kwa maji katika mabwawa makubwa ya kuzalisha umeme
ya Kidatu na Mtera ambayo yalitokana na uharibifu wa vyanzo vya maji katika
maeneo ya juu ya mabwawa hayo.
Aliongeza kuwa ni vema kila mtu
akishiriki kikamilifu katika kuhakikisha kuwa mipango ya matumizi ya maji
yanaratibiwa vyema kisekta ili kuepuka migogoro mikubwa ya watumiaji wenyewe
kwa wenyewe na hata kisekta.
Awali maadhimisho hayo yalitanguliwa na
maandamano makubwa yaliyowashirikisha wadau wa maji na wafanyakazi wa Mamlaka
ya maji na usafi wa mazingira Mbeya pamoja na watumishi wa Bonde la ziwa rukwa.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment