Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, March 9, 2014

KAMPUNI ya vinywaji baridi ya Cocacola Kanda ya Nyanda za juu kusini imeungana na Dunia nzima kuadhimisha Siku ya Wanawake duniani




Meneja masoko wa Cocacola Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Rashid Mgonja alisema  kampuni hiyo pamoja na kuungana na Watanzania katika kuadhimisha siku ya Wanawake duniani pia wamezindua kampeni inayojulikana kwa jina la Good time na Cocacola





Mwanamke Hadhara Njelya mwenye uwezo wa kuchezea mpira jinsi atakavyo kutoka Jijini Mbeya.

Add caption


KAMPUNI ya vinywaji baridi ya Cocacola Kanda ya Nyanda za juu kusini imeungana na Dunia nzima kuadhimisha Siku ya Wanawake duniani kwa kuandaa burudani kubwa iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi RuandaNzovwe Jijini Mbeya.

Burudani hizo zilipambwa na Wasanii kutoka ndani ya Mkoa wa Mbeya walioonesha vipaji vyao akiwemo Mwanamke Hadhara Njelya mwenye uwezo wa kuchezea mpira jinsi atakavyo kutoka Jijini Mbeya.

Mbali na vipaji hivyo vya Mkoa wa Mbeya pia burudani kabambe zilitolewa kutoka kwa wasanii wakubwa wa Jijini Dar Es Salaam ambao ni pamoja na Wasanii kutoka kundi la Wanaume Chege na Temba pamoja na Madee  huku mwendesha sherehe (MC)akiwa ni mtangazaji wa kituo cha Redio cha Clouds fm kipindi cha XXL, B12.

Akizungumzia tukio hilo, Meneja masoko wa Cocacola Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Rashid Mgonja alisema  kampuni hiyo pamoja na kuungana na Watanzania katika kuadhimisha siku ya Wanawake duniani pia wamezindua kampeni inayojulikana kwa jina la Good time na Cocacola.

Alisema lengo la kampeni hiyo ni kujenga mahusiano, kuwaunganisha Watanzania na kuwajengea uwezo wajasiliamali wadogo kupitia vinywaji vya Cocacola kutokana na kuuza bidhaa hizo kwenye maduka yao ambapo kampuni hiyo itaweza kuwapa Majokofu na vifaa vingine vya kufanyia biashara.

Mgonja alisema Kampeni hiyo ni ya Kitaifa ambayo ilianza rasmi Februari 16, Mwaka huu ambapo Kampuni hiyo imejiwekea mikakati kuhakikisha hadi Mwaka 2015 inawanufaisha wajasiliamali wapatao 30,000 kwa Kanda ya Nyanda za Juu pekee ambapo hadi sasa imewanufaisha wajasiliamali 15,000.

Na Mbeya yetu




No comments: