Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, February 3, 2014

SIKU YA SHERIA NCHINI YAFANA MBEYA


Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Mbeya, Noel Chocha,akikagua gwaride la kikosi cha FFU katika kuadhimisha siku ya sheria nchini



Mahakimu na Mawakili wa serikali pamoja na watumishi wa mahakama wakimsikiliza jaji


Waalikwa mbali mbali walikuwepo katika siku ya sheria nchini


Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Mbeya, Noel Chocha, akihutubia waalikwa katika siku ya sheria nchini

Mkuu wa mkoa Mbeya Abasi Kandoro  akitoa neno la shukrani katika siku ya sheria nchini

Msajili wa Mahakama kuu kanda ya Mbeya, Aaron Lyamuya, akitoa taarifa fupi ya maadhimisho ya siku ya sheria nchini

Shekh  wa mkoa Mbeya Mohamed  Ally akisoma dua

Askofu mkuu wa EAGT Mwaisabila 

Askofu Samson Mwalyego
Kwaya ya Baby TOT ikitumbuiza ukumbini 

Kwaya ya mahakama





IMEELEZWA kuwa Tamaa ya baadhi ya viongozi ya kujiingiza katika kila eneo ni kiini na sababu ya vurugu zinazotokea kila wakati baina ya watendaji na wananchi, hivyo kuhatarisha hali ya usalama wa Taifa.

Hayo yamebainishwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Mbeya, Noel Chocha, wakati akizungumza katika maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Sheria Nchini zilizofanyika jana kimkoa katika Ukumbi wa Mahakama kuu kanda ya Mbeya.

Jaji Chocha alisema baadhi ya Viongozi wamekuwa wakijiingiza katika maeneo ambayo siyo taaluma yao hivyo kukosa ufanisi wa kutatua baadhi ya changamoto ambazo hupelekea kupatikana kwa maamuzi mabaya yanayosababisha vurugu katika jamii kwa kukosa Weredi wa jambo husika.

Alisema Ibara ya 107A(1)(2)(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema Mamlaka yenye kauli ya mwisho ya utoaji wa haki katika Jamhuri itakuwa ni Mahakama na katika kutoa uamuzi wa mashauri ya madai na jinai kwa kuzingatia sheria Mahakama ndizo zinaweza kufuata kanuni,na ndiyo msingi wa mgawanyo wa madaraka.

Alisema wapo viongozi wanaokiuka maagizo ya mgawanyo wa madaraka ambapo kwa mujibu wa katiba Mtawala anatakiwa kubaki na jukumu la utawala na Mbunge abaki katika majukumu kadri kadri yanavyoainishwa kupitia ibara ya 63 na 64.

Jaji Chocha alitolea mfano mauaji yaliyotokea wakati wa Operesheni ya Tokomeza ujangiri kuwa ilitokana na baadhi ya viongozi kushika mambo mawili kwa wakati mmoja ingawa nia ya zoezi hilo lilikuwa jema kutokana na wananchi wengi kutofurahishwa na vitendo vya ujangiri ambapo aliwataka viongozi kuwa makini wakati wa kuratibu mikakati ya kukabiliana na ufisadi kwa kutumia Sheria vizuri.

Aliongeza kuwa vita dhidi ya ujangili iwe ya kitaifa kwa kuwahusisha wananchi wote na kwamba vita hiyo inaweza kudhibitiwa kwa kukomesha wimbi la uhamiaji haramu ambao asilimia kubwa wanaonekana kufadhiliwa na nchi kubwa ambazo raia wake wanajihusisha moja kwa moja na biashara za usafirishaji wa Nyara za Serikali hususani meno na pembe za ndovu.

Kwa upande wake Msajili wa Mahakama kuu kanda ya Mbeya, Aaron Lyamuya, Alisema Mahakama imejipanga kuendana na mfumo wa matokeo makubwa sasa(BRN) kwa kujiwekea mikakati mbali mbali inayoendana na kauli mbiu isemayo ‘‘utendaji haki kwa wakati” ambapo Mwaka uliopita Mahakama kuu iliweza kupokea Kesi 429 lakini ilisikiliza na kutoa uamuzi kwa kesi 575 hivyo kuzidi idadi ya kesi ilizopokea.

Alisema katika kipindi cha Mwaka huu mpya ulioanza jana Mahakama kuu kanda ya Mbeya imepanga kusikiliza na kutolea uamuzi kesi walizopokea ambazo ni 670 ingawa kuna changamoto kubwa ya upungufu wa majaji, ambapo hadi sasa Kanda ya Mbeya ina majaji wawili mpaka sasa na kuomba Serikali kuwaongeza ili kuendana na kasi ya kumaliza kesi kwa wakati.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro ambaye alikuwa Mgeni wa Heshima katika sherehe hizo aliipongeza Mahakama kwa kumaliza kesi kwa wakati na kuongeza kuwa Wananchi wanapaswa kuwa na imani na mahakama ili kupunguza migogoro isiyokuwa ya lazima.

Alisema Haki si lazima ipatikane Mahakamani bali zianzie kwenye jamii jambo ambalo pia litasaidia kupunguza mlundikano wa kesi na kujichukulia sheria mikononi baada ya washtakiwa kupelekwa mahakamani na kuachiwa kutokana na maamuzi ya Mahakama lakini kutokana na kutoamini maamuzi hayo hujichulia sheria Mkononi kwa kuamua vinginevyo.

Na Mbeya yetu

No comments: