Picha ya pamoja
KAMPUNI ya Bia Tanzania(TBL) kupitia
kinywaji chake cha Safari imeaandaa mafunzo kwa vijana wanaochoma nyama katika
Mabaa yatakayowawezesha kuingia katika mashindano.
Akizungumzia lengo la kutoa mafunzo kwa
waandaaji wa Nyama choma kwenye mabaa, Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia
Tanzania(TBL) kanda ya Mbeya na Rukwa, Cloud Chawene, alisema kampuni imegundua
kuwa wamiliki wa baa wanategemea Nyama kama moja wapo ya vitu vya kuongeza
mapato yao.
Alisema kutokana na hali hiyo wakaona ni
vema wakaendesha Semina kwa wachoma nyama ili waweze kukidhi vigezo vya
mahitaji ya Wateja ili waweze kufurahia Nyama choma kama ilivyo kwa vyakula
vingine ili kuendana na kauli Mbiu ya Bia ya Safari isemayo“ Safari Lager bila
nyama choma haijakamilika.”
Aliongeza kuwa baada ya mafunzo hayo
yaliyotolewa kwa Baa 42 ambao wametunukiwa vyeti vya ushiriki pia
kutakuwa na mashindano ya kuchoma nyama ambapo washindi 10 watapatikana
kutokana na watakaofuzu vigezo na masharti waliyopewa katika semina hiyo.
Alisema Fainali za Mashindano
zitafanyika Machi 3, Mwaka huu katika Viwanja vya Shule ya Msingi RuandaNzovwe
ambapo washindi watapewa zawadi kuanzia mshindi wa kwanza atakayejinyakulia
Shilingi Milioni moja, mshindi wa pili Laki nane, Mshindi wa tatu Laki 6,
Mshindi wa nne laki nne na Mshindi wa Tano shilingi laki mbili huku mshindi wa
Sita hadi wa Kumi watajinyakulia kifuta jasho cha shilingi 50,000/=.
Alisema namna ya kuwapata washindi ni
kutokana na wateja kupiga kura katika utaratibu utakaobandikwa katika Baa
shiriki ambapo mteja atapiga kura kupitia simu ya mkononi ili kuichagua baa
inayochoma nyama vizuri.
Aliongeza kuwa baada ya zoezi hilo
kukamilika katika Mkoa wa Mbeya itaendelea katika Mikoa mingine ambayo ni
Mwanza, Kilimanjaro,Arusha na Dar Es Salaam mikoa ambayo imetajwa kuwa ndiyo
vinara wa uchomaji nyama pamoja na kuongoza kwa mauzo ya bia ya Safari tofauti
na maeneo mengine.
Kwa upande wake Mkufunzi wa Mafunzo
hayo, Laurence P. Salv ambaye pia ni Jaji Mkuu wa mashindano hayo amesema
huwezi kuandaa mashindano bila ya kutoa Elimu.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment