Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, February 10, 2014

SAFARI LAGER NYAMA CHOMA YAIVA JIJINI MBEYA

Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kanda ya Mbeya na Rukwa, Cloud Chawene, alisema kampuni imegundua kuwa wamiliki wa baa wanategemea Nyama kama moja wapo ya vitu vya kuongeza mapato yao.

Mkufunzi wa Mafunzo hayo, Laurence P. Salv ambaye pia ni Jaji Mkuu wa mashindano hayo amesema huwezi kuandaa mashindano bila ya kutoa Elimu.


Moja ya washiriki ya semina ya safari nyama choma akipokea cheti cha mafunzo

Picha ya pamoja

KAMPUNI ya Bia Tanzania(TBL) kupitia kinywaji chake cha Safari imeaandaa mafunzo kwa vijana wanaochoma nyama katika Mabaa yatakayowawezesha kuingia  katika mashindano.

Akizungumzia lengo la kutoa mafunzo kwa waandaaji wa Nyama choma kwenye mabaa, Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kanda ya Mbeya na Rukwa, Cloud Chawene, alisema kampuni imegundua kuwa wamiliki wa baa wanategemea Nyama kama moja wapo ya vitu vya kuongeza mapato yao.

Alisema kutokana na hali hiyo wakaona ni vema wakaendesha Semina kwa wachoma nyama ili waweze kukidhi vigezo vya mahitaji ya Wateja ili waweze kufurahia Nyama choma kama ilivyo kwa vyakula vingine ili kuendana na kauli Mbiu ya Bia ya Safari isemayo“ Safari Lager bila nyama choma haijakamilika.”

Aliongeza kuwa baada ya mafunzo hayo yaliyotolewa kwa Baa 42 ambao wametunukiwa vyeti vya ushiriki  pia kutakuwa na mashindano ya kuchoma nyama ambapo washindi 10 watapatikana kutokana na watakaofuzu vigezo na masharti waliyopewa katika semina hiyo.

Alisema Fainali za Mashindano zitafanyika Machi 3, Mwaka huu katika Viwanja vya Shule ya Msingi RuandaNzovwe ambapo washindi watapewa zawadi kuanzia mshindi wa kwanza atakayejinyakulia Shilingi Milioni moja, mshindi wa pili Laki nane, Mshindi wa tatu Laki 6, Mshindi wa nne laki nne na Mshindi wa Tano shilingi laki mbili huku mshindi wa Sita hadi wa Kumi watajinyakulia kifuta jasho cha shilingi 50,000/=.

Alisema namna ya kuwapata washindi ni kutokana na wateja kupiga kura katika utaratibu utakaobandikwa katika Baa shiriki ambapo mteja atapiga kura kupitia simu ya mkononi ili kuichagua baa inayochoma nyama vizuri.

Aliongeza kuwa baada ya zoezi hilo kukamilika katika Mkoa wa Mbeya itaendelea katika Mikoa mingine ambayo ni Mwanza, Kilimanjaro,Arusha na Dar Es Salaam mikoa ambayo imetajwa kuwa ndiyo vinara wa uchomaji nyama pamoja na kuongoza kwa mauzo ya bia ya Safari tofauti na maeneo mengine.

Kwa upande wake Mkufunzi wa Mafunzo hayo, Laurence P. Salv ambaye pia ni Jaji Mkuu wa mashindano hayo amesema huwezi kuandaa mashindano bila ya kutoa Elimu.

Na Mbeya yetu

No comments: