Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, February 4, 2014

MORAVIANI JIMBO LA KUSINI MAGHARIBI WAVURUGANA

Mchungaji Chilale Edward Simoni kuwa Mwenyekiti wao na 

Daudi Mwiligumo akisoma  tamko waliloliandaa linalopinga maamuzi ya kusimamishwa uongozi Mwenyekiti wao wa Jimbo na kuitaka Mahakama kuingilia kati.


Baadhi ya Wachungaji wapatao 25 wa kanisa hilo walijitokeza mbele ya vyombo vya habari wakitoa tamko kali la kuutaka kurejeshewa kwa madaraka yake Mwenyekiti huyo ili kunusuru kuvunjika kwa kanisa.


HILI NDILO TAMKO LA WACHUNGAJI 25 ENDELEA KUSOMA







KANISA la Morovian Jimbo la Kusini Magharibi lenye makao makuu Mkoani Mbeya limeingia katika mgawanyiko mkubwa baada ya viongozi, Wachungaji na Waumini kutoelewa kutokana na kuvuliwa uongozi kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Jimbo hilo.

Mwenyekiti aliyesimamishwa uongozi ni Mchungaji Nosigwe Buya ambapo baadhi ya Watumishi, Waumini na Wachungaji wa Kanisa hilo kupinga maamuzi ya kuondolewa kwa Mwenyekiti kwa madai kuwa maamuzi hayo yalikiuka katiba ya katika.

Kutokana na kuwepo kwa mtafaruku ndani ya kanisa hilo, Baadhi ya Wachungaji wapatao 25 wa kanisa hilo walijitokeza mbele ya vyombo vya habari wakitoa tamko kali la kuutaka kurejeshewa kwa madaraka yake Mwenyekiti huyo ili kunusuru kuvunjika kwa kanisa.

Wachungaji hao ambao walimchagua Mchungaji Chilale Edward Simoni kuwa Mwenyekiti wao na Daudi Mwiligumo kusoma tamko waliloliandaa linalopinga maamuzi ya kusimamishwa uongozi Mwenyekiti wao wa Jimbo na kuitaka Mahakama kuingilia kati.

Akisoma tamko hilo, Mchungaji Mwiligumo alisema jambo wanalopingana nalo ni  pamoja na kikao cha kumsimamisha Mwenyekiti kilivunja katiba ya kanisa iliyosahihishwa na kusanifiwa mwaka 2012 ibara ya 11 kifungu cha 4(iv).

Alisema kifungu hicho kinasema Mwenyekiti asipokuwepo, Makamu mwenyekiti atakuwa mbadala yake na ibara ya 35 inasema wakati wowote Mwenyekiti asipokuwepo Makamu atakuwa Mwenyekiti lakini katika kikao kilichomuondoa Mwenyekiti wao hata Makamu hakuwepo hivyo kikao kilikosa uongozi.

Aliongeza kuwa katika kikao kilichofanyika Julai 31, Mwaka jana kilimuondoa Katibu Mkuu ambaye kwa mujibu wa Katiba ibara ya 36(2)(ii) ambacho kinataja moja ya kazi za katibu ni kuandika Muhtasari wa kikao  hivyo kikao hicho hakikua halali kutokana na watendaji wakuu kutokuwepo.

Tamko hilo liliendelea kudai katiba ya kanisa hilo iliendelea kuvunjwa baada ya Muumini wa kawaida aliyetajwa kwa jina la  Charles Mwakipesile kukalia kiti kinyume cha ibara ya 10(2)C ambacho kinasema Mwenyekiti na makamu sharti wawe wachungaji.

Walisema kwa mujibu wa katiba mwenyejukumu la kumuondoa kiongozi yeyote katika nafasi yake ni Mkutano mkuu wa Sinodi unaohusisha wajumbe wengi na kwamba Mwenyekiti aliyeondolewa alichaguliwa kihalali na Sinodi mwaka 2012.

Mbali na hilo wachungaji hao walidai vipengere vingine kukiukwa ni pamoja na kumdalisha kazi Mwenyekiti huyo kinyume na utaratibu ikiwa ni pamoja na kumpangia katika kituo kipya cha kazi ambayo ni ya chini kuliko wadhifa aliyokuwa nao.

Pia walipinga kitendo cha Kutakiwa Mwenyekiti huyo kuhama katika nyumba za kanisa hadi kufikia Februari 7, Mwaka huu kinyume cha utaratibu uliwekwa na kanisa hiloambao kila kiongozi wa Kamati tendaji hutakiwa kuishi katika nyumba zilizo ndani ya Makao makuu ya Jimbo.

Waliongeza kuwa juhudi zao zote ni kutaka kulinusuru kanisa na kuiomba Mahakama na vyombo vya Dola kuingilia kati kwa kumtambua Mwenyekiti wa Jimbo Mchungaji Buya kuwa ndiye Mwenyekiti halali wa Jimbo na kuiamuru Halmashauri ya jimbo na kamati tendaji pamoja na Askofu Alinikisa Cheyo kuitisha Mkutano wa Sinodi haraka kwa ajili ya maamuzi.

Aidha mgogoro unaoendelea ndani ya kanisa hilo pia umemhusisha moja kwa moja Askofu wa jimbo hilo, Alinikisa Cheyo na kwamba kuna watu wachache wanataka kulitumia kanisa kama taasisi binafsi kujinufaisha wao wenyewe.

Kwa upande wake Askofu wa Kanisa hilo ambaye yuko safarini Nchini Kenya, Alinikisa Cheyo alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusiana na jambo hilo alionesha kusikitishwa na hatua ya wachungaji kukimbilia kwenye vyombo vya habari kwa madai kuwa hilo jambo bado liko kwenye mazungumzo.

Alisema pamoja na yeye kuhusishwa na jambo hilo bado wachungaji pia wamekiuka katiba kutokana na kumpelekea malalamiko ambayo hayana mihutasari ya kikao chao pamoja na sahihi za wachungaji waliokusanyika kufanya kikao hicho.

Alisema hata jambo wanalozungumzia linamhusu mtu mmoja ambaye ni Mwenyekiti hivyo kutumia cheo kimoja kuivura taasisi nzima ni makosa ili hali Mwenyekiti huyo amesimamishwa tu na sio kufukuzwa na kwamba aliyesimamishwa anao uwezo wa kukata rufaa kupinga maamuzi hayo.

Aliongeza kuwa milango ya mazungumzo iko wazi hivyo sio busara kwa wachungaji kutoka nje ya kanisa na kuwaeleza watu wengine na kuongeza kuwa Sinodi wanayoshauri kuitishwa hakuna shida yoyote kwamba muda wowote wakitaka wataitisha.

Na Mbeya yetu

3 comments:

Anonymous said...

Askofu yupo ambaye anauwezo wa kushauri migogoro katika jimbo. Wachungaji pia hawakua sahihi kukimbilia katika vyombo vya habari na kuomba msaada wa mahakama. Askofu Cheyo ziba ufa kabla ya kujenga ukuta

Anonymous said...

Askofu Cheyo tatua mgogoro kabla halijawa tatizo kubwa

Anonymous said...

CHEYO ULISHAURIWA MAPEMA KUUMALIZA HUO MGOGORO MAPEMA LAKINI HUKUTAKA,LEO UNAWALAUMU WACHUNGAJI ULITAKA WAENDE WAPI,KAMA UMEONA LIMEKUWA GUMU LUDI UMALIZE P