Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ndg. Mbarak Abdulwakil
anatarajia kuzindua rasmi Magereza "Duty Free Shop" - Ruanda, Mbeya
kesho saa 3:30 asbuhi Februari 12, 2014 katika Viwanja vya Ofisi ya
Magereza Mkoa wa Mbeya ambapo shughuli hiyo itashuhudiwa na Viongozi
mbalimbali toka Ofisi za Serikali, Binafsi pamoja na Wananchi wanaoishi
jirani na maeneo ya Gereza Kuu Ruanda, Mbeya.
Mpango
huu wa ujenzi wa Magereza "Duty Free Shops" katika Mikoa ya Kimagereza
Kiutawala unatekelezwa kwa Mafanikio makubwa na Uongozi wa Jeshi la
Magereza unaosimamiwa kimkakati na Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza, John Casmir Minja hivyo kutimiza adhima ya Serikali ya Awamu
ya Nne ya kuwasogezea huduma za bidhaa muhimu na zenye manufaa Maafisa,
Askari wa Jeshi la Magereza pamoja na familia zao katika maeneo yao ya
kazi.
Aidha,
mpaka sasa jumla ya "Duty Free Shops" tano (05) zimezinduliwa sehemu
mbalimbali hapa nchini hususani katika Mikoa ya Dar es Salaam(Ukonga),
Dodoma(Gereza Isanga), Morogoro(Chuo cha Ufundi na Udereva Kingolwira),
Kilimanjaro(Gereza Karanga, Moshi) na Mwanza(Gereza Butimba).
Kuzinduliwa
kwa Magereza "Duty Free Shop" - Ruanda, Mbeya kunafanya idadi yake
kuongezeka na kufikia jumla ya Magereza "Duty Free Shop" sita(06) ambazo
zimekamilika hapa Nchini katika Mikoa ya Kimagereza Kiutawala.
Vyombo
vya Habari ikiwa wadau muhimu katika dhima ya kuuhabarisha umma
vinakaribishwa kwenye tukio la uzinduzi rasmi wa Magereza "Duty Free
Shop" - Ruanda, Mbeya kesho Februari 12, 2014 kuanzia saa 3:30 asbuhi
katika Viwanja vya Ofisi za Magereza Mkoa wa Mbeya.
Imetolewa na;
Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Mbeya
Februari 11, 2014.
No comments:
Post a Comment