|
Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Ahmed Msangi
Watu watatu
wamefariki dunia mkoani Mbeya katika matukio matatu tofauti yaliyotokea mkoani
hapa.
Tukio la
kwanza limetokea majira ya saa tano asubuhi katika Hospitali ya Rufaa Jijini
Mbeya ambapo Huruma Laiton[20]mkazi wa Kijiji cha Inyala Kata ya Iyunga kufariki
dunia akipatiwa matibabu baada kupigwa na mumewe aitwaye Ezekiel
Mwakabenga[21].
Kamanda wa
Polisi mkoani Mbeya Ahmed Msangi amesema kuwa chanzo cha mauaji ni wivu wa
kimapenzi kwani imedaiwa kuwa marehemu alikutwa akifanya mapenzi na mtu
mwingine majira ya saa kumi alfajiri Januari mosi mwaka huu katika nyumba yake.
Mama mwenye
nyumba walimokuwa wanaishi wanandoa hao Rose Mwembe baada ya kusikia ugomvi
alienda kutoa taarifa kwa Balozi wa mtaa Asajile Kandonga ambapo baada ya
kufika na kukuta hali ya marehemu ni mbaya walimkimbiza Hospitali ya Rufaa
ndipo alifariki akipatiwa matibabu.
Mtuhumiwa
amekatwa na atafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika,aidha mwili
wa marehemu umezikwa nyumbani kwao Inyala Januari 2 mwaka huu.
Katika tukio
la pili Msangi amesema Christopher Myamba[20]mkazi wa Nsalaga ameuwa kwa
kuchomwa nakisu shingoni na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la
Ndele,chanzo cha mauaji ni mzozo uliotokea baada ya marehemu na rafiki yake
aitwae Baraka Mwalatu kukutana njiani marehemu akiwa na baiskeli Ndele na
wenzake walikataa kupisha njia na kumchoma kisu marehemu.
Mtuhumiwa
alitoroka mara baada ya tukio na Kamanda Msangi ametoa wito kwa yeyote mwenye
taarifa alipo mtuhumiwa akamatwe achukuliwe hatua za kisheria.
Wakati huo
ho mtu mmoja aliyefamika kwa jina la Nnanzala Mayala[60] amefariki baada ya
kukatwa katwa na vitu vyenye ncha kali na mtu au watu wasiofahamika katka
kijiji cha Simike Wilaya ya Mbarali.
|
Hakuna mtu
aliyekamatwa na chanzo cha mauaji hakijafahamika.
No comments:
Post a Comment