Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, January 9, 2014

MKUU WA WILAYA YA RUNGWE MH.CHRISPIN MEELA AONGOZA WANANCHI KATIKA MAZISHI YA ASKARI WA USALAMA BARABARANI S/STG BENADETHA OLOMI ALIYEFARIKI AKIWA KAZINI KWA KUGONGWA NA GALI ENEO LA MCHANGANI TUKUYU WILAYANI RUNGWE


MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA AKITOA SALAM ZA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA YA MAREHEMU NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA HASA WILAYA YA RUNGWE PIA KWA WANANCHI WOTE KWA KUSHITUSHWA NA KIFO CHA ALIYEKUWA ASKALI KATIKA KITENGO CHA USALAMA WA BARABARANI BENADETHA OLOMI (MAMA) BAADA YA MAUTI KUMKUTA AKIWA KAZINi MCHANGANI - ISONGOLE AMBAPO ALIGONGWA NA GARI ALIPOKUWA KASIMAMISHA GARI LINGINE LILILOKUWA LINATOKEA MBEYA KWENDA TUKUYUNDIPO GARI LINAENDESHWA NA ELNEST NDOA KUTOKA WILAYA YA KYELA LIKAMGONGA NA KUSABABISHA KIFO PAPO HAPO. HIVYO CHRISPIN MEELA AMEWATAKA MADELEVA KUACHA KUENDESHA KWA KASI MAGARI SEHEMU ZA MAKAZI YA WATU NA SEHEMU ZA VITUO WANAPO SIMAMA ASKALI WA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZISIZO
ZA LAZIMA

1962 - 2014

MISA YA MAZIKO IMEFANYIKA KATIKA PAROKIA YA TUKUYU AMABAPO MAREHEMU ALIKUWA MWANA KWAYA. MISA IMEONGOZWA NA PAROKO MSAIDIZI PROJESTUS KAHITWA AMABAPO AMEWATAKA WATU KUJIANDAA KWA SAFARI YA MBINGUNI KWA KUWA WATENDA MEMA HAPA DUNIANI KWANI HAKUNA AJUAYE SAA WALA DAKIKA YA KUFARIKI KWAKE HIVYO MUHIMU NI KUJIANDAA

BAADHI YA WATOTO WA MAREHEMU WAKIWA IBADANI KWA AJILI YA MISA YA KUMUOMBEA MAREHEMU MAMA YAO

KULIA PAROKO MSAIDIZI PROJESTUS KAHITWA AKIONGOZA MISA YA KUMUOMBEA MAREHEHEMU BENADETHA OLOMI


MUME WA MAREHEMU MR EZEKEEL  KALABAN MWANDETELE

WATOTO WAMAREHEMU WAKITOA HESHIMA ZAO ZA MWISHO KWA MAREHEMU MAMA YAO KIPENZI



ASKOFU WA DAYOSISI YA KONDE KKKT DR ESRAEL MWAKYOLILE AKITOA HESHIMA ZA MWISHO

AFISA USALAMA WA TAIFA WILAYA YA RUNGWE AKITOA HESHIMA ZA MWISHO


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA AHMED MSANGI AKIWEKA UDOGO KATIKA KABURI LA MAREHEMU BENADETHA OLOMI


HESHIMA ZA MWISHO ZA KIJESHI BAADA YA MAZIKO



HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREHEMU
KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AHMED MSANGI AMEWATAKA NDUNGU NA JAMAA KUWA NA MOYO WA UVUMILIVU KWA KIPINDI HIKI KIGUMU SANA KWANI ALIYETUPA BENADETHA NDIYE ALIYETUPA PIA AMESEMA KUWA HAKI ZOTE ZA MAREHEMU ZITAPATIKANA NA WATOTO NA MUMEWE WA MAREHEMU WATAKABIDHIWA

UFAFANUZI WA JINA LA MAMA AMBALO NI MAARUFU KWA MAREHEMU BENADETHA ULIANZIA KWA MWENYEKITI WA KIJIJI CHA SYUKULA AMBAPO MZEE NASSORO HUMBO AMESEMA BENADETHA ALIKUWA MTU WA HURUMA NA MOYO WA KIPEKEE KWAKUWA KILA MTU WA KIJIJI HIKI AKIUMWA AU ANASHIDA YEYE AKIWA TUKUYU ATASAIDIA MATIBABU NA KUPATA POSHO PIA AMBALO HATASAULIKA KIJIJINI NI KUANZISHA MRADI WA MAJI SAFI HIVYO MARADI AMBAO UMEFANYA KIJIJI SASA KUWA NA MAJI AMBAYO SASA HATA VIJIJI VYA JIRANI WANAPATA MAJI

IBADA YA MAZIKO IKAFUNGWA KWA KUWASHA MISHUMAA KATIKA KABURI LA MAREHEMU BENADETHA OLOMI ALIYEZALIWA MWAKA 1962 NA ALIANZA KAZI KATIKA JESHI LA POLISI MWAKA 1982 NA AMEFARIKI AKIWA NA CHEO CHA S/SGT AKIWA ASKARI WA USALAMA BARABARANI. MAREHEMU AMEACHA MUME MMOJA NA WATOTO WATANO NA WAJUKUU WAWILI


No comments: