Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, January 10, 2014

Madiwani wametakiwa kutowatuhumu watendaji wa Halmashauri au wataalamu wanaofanya kazi Wilayani Mbozi kwa ubadhilifu bila kuwa na ushahidi wa kutosha.

Katibu wa Baraza Kaimu Mkurugenzi Daktari Charles Mkombachepa akiongea na madiwani    
 Katikati Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi Ambakisye Minga 
Madiwani wakichangi Hoja
Danny Tweve afsa Tehama wilaya ya Mbozi akifafanua jambo fulani
Wakuu wa idara

Madiwani wametakiwa kutowatuhumu watendaji wa Halmashauri au wataalamu wanaofanya kazi Wilayani Mbozi kwa ubadhilifu bila kuwa na ushahidi wa kutosha.

Kauli hiyo ameitoa Katibu wa Baraza Kaimu Mkurugenzi Daktari Charles Mkombachepa ambaye amesema hayo katika kikao cha Baraza la Madiwani wa wilaya ya Mbozi kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri Januari 8 mwaka huu.

Kikao hicho kilikuwa kinapitisha mapendekezo ya Bajeti ya Halmashauri hiyo ambapo Halmashauri inatarajia kutumia zaidi Bilioni 44 kutokana na vyanzo mbalimbali na wafadhili.

Mkombachepa amesema kuwa baadhi ya waheshimiwa wamekuwa wakiwatuhumu wataalamu  bila kuwa na vieelezo na ushahidi wa kutosha na hivyo kuwavunja moyo na wengine kuamua kuomba uhamisho na hivyo kufanya wilaya hiyo kukosa wataalamu wa kutosha.

Amesema kuwa endapo watakuwa na ushahidi wa kutosha wawasiliane na ofisi yake itakuwa tayari kutoa msaada ili kuleta maendeleo katika wilaya ya Mbozi.

Katika bajeti hiyo kipaumbele kikubwa kimepewa  ujenzi wa kituo cha mabasi Mlowo kitakachogharimu shilingi milioni 600,Ununuzi wa gari la wagonjwa na gari la ukaguzi wa elimu sekondari ambapo kila gari litagharimu shilingi milioni 150,maabara tano za shule za sekondari zitakazo gharimu shilingi milioni 450.

Pia kikao hicho kiliridhia kutumika shilingi milioni 95 kwa ajili ya upimaji wa mipaka kiutawala baada ya kugawanywa  kwa wilaya za Momba na Mbozi.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi Ambakisye Minga amesema kuwa makisio hayo endapo yataridhiwa na ngazi za juu ni vema kuwa na nidhamu ya matumizi ili kila lililokusudiwa lifanyike ili kuleta imani kwa wananchi na serikali kwa ujumla.

Mbeya yetu

No comments: