KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom
Mbeya mjini imetoa msaada wa vitu mbali mbali kwa vituo vitatu vya kulelea
watoto yatima wa zaidi ya Shilingi Milioni tatu.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi
hizo katika hafla iliyofanyika katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Nuru
Orphans Centre kilichopo Uyole Jijini Mbeya, Meneja wa Kampuni hiyo Mbeya mjini
Emmanuel Sagenge amesema kama kampuni imeguswa sana na uwepo wa watoto yatima
katika jamii inayowazunguka.
Amesema kuwa ni vema makampuni
mengine pamoja na taasisi mbali mbali kujenga utamaduni wa kujitolea kwa ajili
ya watotro yatima na sio kluwaachia jukumu hilo wenye vituo pekee kwa sababu
kazi hiyo ni ya jamii nzima ya watanzania.
Amevitaja vitu walivyotoa ambavyo
vinagharimu kiasi cha fedha taslimu shilingi million tatu kuwa ni pamoja na
unga wa sembe gunia 6 zenye ujazo wa kilo sita kila kimoja, sabuni katoni 6,
sabuni za unga ndoo 6, sabuni za vipande miche 6,mafuta ya kula ndoo 6,
mchele kilo 60 na maharage kilo 60.
Vingine ni Peni, kalamu, madaftari,
miswaki, juisi, rula, dawa za miswaki, maziwa na chumvi ambavyo vitagawanywa
katika vituo vyote vitatu kulingana na mahitaji ya vituo vyenyewe.
Kwa upande wake mratibu wa zoezi hilo.
Zahara Mansoor ambaye pia ni Mwenyekiti wa mtandao wa watoto mkoa wa Mbeya
amesema msaada huo utagawanywa katika vituo vitatu ambavyo ni Nuru, Iwambi na
Chipro vyote vya jijini Mbeya.
Amesema huo ni utaratibu wake
aliojiwekea wa kutoa zawadi kwa watoto yatima kila mwaka kupitia makampuni
mbali mbali yanayoguswa na uwepo wa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment