Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, January 12, 2014

KAMPUNI ya Citysign Promotion & Markerting Agency Limited ya Jijini Mbeya inatarajia kuandaa ligi ya mpira wa miguu itayohusisha timu za madereva wa pikipiki maarufu bodaboda za Jiji la Mbeya.

 Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Citysign Promotion & Markerting Agency Limited  Geophrey Mwangunguru katika kikao cha maandalizi baina yao na viongozi wa chama cha waendesha bodaboda kilichofanyika katika viwanja vya City pub Jijini Mbeya.


Baadhi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo

 Mwenyekiti wa kamati ya ufundi wa shirikisho la mpira wa miguu Jiji la Mbeya(MUFA) Ramadhani Lulandala alisema ni vema madereva wa bodaboda wakajiandaa vizuri huku wakitambua sheria na kanuni za mpira wa miguu kwa kuepuka kuwafanyia vurugu waamuzi na kwamba atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.
 Mwenyekiti   wa bodaboda  jiji la Mbeya Vicent Mwashoma 





KAMPUNI ya Citysign Promotion & Markerting Agency Limited ya Jijini Mbeya inatarajia kuandaa ligi ya mpira wa miguu itayohusisha timu za madereva wa pikipiki maarufu bodaboda za Jiji la Mbeya.

Hayo yamebainishwa na mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo, Geophrey Mwangunguru katika kikao cha maandalizi baina yao na viongozi wa chama cha waendesha bodaboda kilichofanyika katika viwanja vya City pub Jijini Mbeya.

Mwaangungulu alisema lengo la kuandaa ligi hiyo ni kuwaunganisha madereva wa bodaboda ili kusudi waweze kutambuliwa na wanajamii  ambao asilimia kubwa wamekuwa wakiwatuhumu kwamba ni wakorofi waliokosa ustarabu na umoja.

Alisema kupitia ligi hiyo wataweza kupata faida kubwa kwa kupatiwa elimu mbalimbali zikiwemo usalama barabarani ili kupunguza ajali zisizokuwa za lazima,kuunganishwa na mifuko ya jamii, bima za afya,saccos na jinsi ya kujiwekea akiba.

Aliongeza kuwa ligi hiyo intarajiwa kuanza kulindima mapema mwezi wa nne baada taratibu zote kukamilika kwa kuzihusisha timu zaidi ya 30 ambazo ni timu tano kutoka kanda sita za vituo vya bodaboda.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya ufundi wa shirikisho la mpira wa miguu Jiji la Mbeya(MUFA) Ramadhani Lulandala alisema ni vema madereva wa bodaboda wakajiandaa vizuri huku wakitambua sheria na kanuni za mpira wa miguu kwa kuepuka kuwafanyia vurugu waamuzi na kwamba atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Aidha kwa upande wao viongozi wa boda boda wakiongozwa na Mwenyekiti wao Vicent Mwashoma na katibu Msumba Mdesa waliwapongeza waandaaji wa ligi hiyo kwa kuwakumbuka waendesha bodaboda na kuwahakikishia kushiriki ligi hiyo kwa amani na kwamba haina haja ya kulihusisha jeshi la polisi kwa madai kuwa wanauwezo wa kudhibitina wao wenyewe.

Na Mbeya yetu

No comments: