Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, January 21, 2014

HALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya imelalamikiwa kwa kuhodhi zaidi ya shilingi milioni 254 zilizotolewa na serikali kuu kwa ajili ya miradi mbalimbali katika mji wa Tunduma kabla ya kuganywa kuwa Halmashauri mbili.

 HALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya imelalamikiwa kwa kuhodhi zaidi ya shilingi milioni 254 zilizotolewa na serikali kuu kwa ajili ya miradi mbalimbali katika mji wa Tunduma kabla ya kuganywa kuwa Halmashauri mbili.

Hayo yalibainishwa juzi na Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Tunduma, Elias Cheyo, alipokuwa akitoa taarifa kwa Katibu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) kata ya Tunduma, Hemed Stephen, alipofanya ziara ya kukagua miradi mbali mbali.

Cheyo alisema kutokana na kutopelekwa kwa fedha hizo kumesababisha kukwama kwa ujenzi wa vyumba 21 vya madarasa ya shule mbalimbali katika kata hiyo.

Baadhi ya shule zilizokumbwa na adha hiyo ni pamoja na Shule ya msingi Mkombozi na Mwaka ambazo zinakabiliwa na changamoto kubwa za msongamano mkubwa wa wanafunzi madarasani.

Cheyo alisema kuwa kukosekana kwa fedha hizo kunawakatisha tamaa wazazi ambao wameweza kujenga madarasa hadi mtambaapanya wakati jukumu la serikali ni kupaua na kumalizia sakafu.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa mji mdogo wa Tunduma wilaya ya Momba,Aidan Mwanshiga alisema ruzuku hiyo ilitumwa Halmashauri mama ya Mbozi ambayo inapaswa kutoa fedha hizo kila mwezi lakini haijafanya hivyo kwa mwaka mmoja sasa.

Mwanshiga alisema kuwa wametafuta fedha nyingine kutokana na vyanzo vya ndani ili kupunguza adha hiyo ya upungufufu wa madarasa ili ifikapo mwezi marchi watoto wote wawe madarasani.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi, Ambakisye Minga alipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo alisema kuwa hana maelezo kuhusiana na jambo hilo atafutwe Mkurugenzi wa Halmashauri yeye ndiye mwenye dhamana ya kujibu masuala ya fedha za Hamashauri.

Hata hivyo juhudi za kumpata Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi Charles Mkombachepa kupitia  simu yake ya kiganjani zilifanikiwa ambapo alijibu  kuwa yupo kwenye kikao.

No comments: