Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, December 13, 2013

Wananchi wa kijiji cha Ruiwa kata ya Ruiwa wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wamemgomea Diwani wa kata hiyo Alex Mdimilaje kuchanga mchango wa ujenzi wa sekondari ya Gwili kutokana na ubadhilifu.

Diwani  Alex Mndimilaje anaedaiwa kufumbia macho ufujaji wa pesa ambapo wamedai kuwa jumla ya shilingi milioni 27 kudaiwa kuibwa na mhasibu wa kijiji John Onyese ambaye ametoroka na hivi sasa anatafutwa na mwajiri wake pia jeshi la Polisi mkoani Mbeya.

Pamoja na juhudi za Katibu kata wa chama cha Mapinduzi kata ya Ruiwa Expeditor Pius Kibang’ole kuwaomba wananchi wakubali kuchanga walikataa wakidai hawana imani na Diwani pamoja na kamati hivyo wapo tayari kukamatwa.




Wananchi wa kijiji cha Ruiwa kata ya Ruiwa wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wamemgomea Diwani wa kata hiyo Alex Mdimilaje kuchanga mchango wa ujenzi wa sekondari ya Gwili kutokana na ubadhilifu.

Kauli hiyo imetolewa na wananchi hao katika mkutano wa hadhara ulofanyika katika kijiji hicho  hivi karibuni kufuatia mkutano wa awali kuahirishwa wakiikataa kamati ya elimu ya kata iliyowataka wananchi kuchangia mchango wa sekondari ya Gwili ambapo watoto 210 wa kata hiyo kufaulu kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza mwaka 2014.

Wananchi hao wamekasirishwa na kitendo cha Diwani kufumbia macho ufujaji wa pesa ambapo wamedai kuwa jumla ya shilingi milioni 27 kudaiwa kuibwa na mhasibu wa kijiji John Onyese ambaye ametoroka na hivi sasa anatafutwa na mwajiri wake pia jeshi la Polisi mkoani Mbeya.

Aidha wananchi hao wamemtuhumu aliyekuwa mtendaji kata Jordan Masweve wakidai kuwa kwa kushirikiana na Diwani wamezorotesha maendeleleo katika kata yao huku wananchi wakiendelea kuchangishwa michango bila kusomewa mapato na matumizi ya sekondari kwa miaka mitatu sasa.

Pamoja na wananchi hao kuombwa na mwenyekiti wa kijiji hicho Hadji Mohammed Dende kuwa watulivu katika mkutano wananchi hao hawakuafiki ombi la Diwani  la kutaka wachangie shilingi elfu tano badala ya elfu kumi ili watoto waanze masomo Januari mwakani lakini wananchi waliendelea kumzomea.

Kwa upande wake Diwani aliendelea kuwaomba wananchi kusamehe mapungufu ya huko nyuma hivyo warudishe moyo ili waeendelee na mchango lakini wananchi walikataa wakidai hivi sasa hawana pesa na ni msimu wa kilimo.

Pamoja na juhudi za Katibu kata wa chama cha Mapinduzi kata ya Ruiwa Expeditor Pius Kibang’ole kuwaomba wananchi wakubali kuchanga walikataa wakidai hawana imani na Diwani pamoja na kamati hivyo wapo tayari kukamatwa.

Wamesema kuwa malalamiko yao wamefikisha kwenye ofisi ya mkurugenzi na mkuu wa wilaya ya Mbarali lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa hivyo wanamtaka mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro kutatua mgogoro huo na kuikoa kata hiyo na migogoro ya mara kwa mara.

Mkutano huo ulimalizika bila utaratibu wa kawaida na wananchi kumzomea Diwani huku wakirushiana maneno makali.

Na Ezekiel Kamanga 
Mbeya yetu


No comments: