Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, December 1, 2013

TBL MBEYA WAADHIMISHA SIKU YA UKIMWI DUNIANI KWA KUPIMA UKIMWI NA AFYA ZAO KWA UJUMLA

Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Mbeya wakijiandaa kwenda kupima ukimwi ili kuungana na wenzao Duniani kote katika maadhimisho ya siku ya ukimwi Duniani
Moja ya wafanayakazi wa TBL Mbeya akipimwa ukimwi kiwandani hapo
Baadhi ya wafanayakazi wa TBL Mbeya wakiwa wamepanga mstari kusubiri zamu zao ya kupima
Mratibu wa usalama na afya kazini wa TBL Mbeya  Misana Misana  alisema, wamechukua uamuzi wa  kupima ukimwi ili kuhamasisha jamii kujitokeza kupimwa ugonjwa huo.
Baada ya yazoezi la kupimwa ukimwi wafanayakazi wa TBL wanarudi kuendelea na kazi


TBL MBEYAAkizungumza na waandishi wa, habari  mratibu wa usalama na afya kazini wa TBL Mbeya  Misana Misana  alisema, wamechukua uamuzi wa  kupima ukimwi ili kuhamasisha jamii kujitokeza kupimwa ugonjwa huo.
       Alisema, ipo haja ya wananchi kuendelea kuhamasishwa kwa njia mbalimbali kupima afya zao kwa kuwa bado wapo ambao bado wanaogopa au kuona aibu kwenda kupimwa ukimwi kutokana na sababu mbalimbali.
     "Hatua ya kujitokeza kwa wafanayakazi wa TBL Mbeya kupimwa itakuwa hamasa kubwa kwa watu wengine na pia itasaidia wafanyakazi wenyewe kutambua afya zao na hivyo kuchagua kwa usahihi aina ya maisha watakayoishi katika kupambana na ukimwi.

Na Mbeya yetu

No comments: