Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, December 28, 2013

HOT NEWS…….NDOA YAVUNJIKA RASMI WAVUTANA KURUDISHIANA FEDHA WALIZOPOKEA.

Bwana harusi akiwa na mpambe wake kanisani wakimsubiri bibi Harusi
Jamaa wameshika vichwa hali haieleweki
Bi Harusi Naomi Ngoje akiwa amejilalia chumbani akiwa anahuzunika na kushangaa wazazi wake kurudisha mahali ya mchumba wake


HABARI zilizotufikia hivi punde kutoka nyumbani kwa familia ya Bi harusi ambayo ilikuwa ikipinga ndoa isifungwe kutokana na Bwana harusi kushindwa kumalizia sehemu ya Mahari zinadai kuwa ndoa imevunjwa rasmi na kilichobaki ni mzozo wa kurudishiana fedha.

Pande hizo mbili ya Kiume na Kike zimengia kwenye Mzozo na kuvutana kuhusu fedha baada ya Wazazi wa Mwanamke kukubali kurudisha fedha hizo pamoja na vitu walivyopokea huku kikubwa kikiwa ni upande wa Mwanaume kudai wapewe papo hapo.

Vitu vinavyodaiwa ni Fedha taslimu takribani Shilingi 310,000/= ambazo zilitolewa kwa ajili ya Mkaja pamoja na kiingilio, Blanketi na Mashuka.

Kwa habari zaidi endelea kufuatilia mtandao wako kila wakati unaokupa habari zisizoacha shaka kwa msomaji.

NaMbeya yetu

2 comments:

Anonymous said...

Masikini Ndugu Mahenge. Anatisha huruma sana. Sio neno baba. Utapata mwingine tu. Achana na hiyo familia. Kama huyo mchumba wako unampenda saaaana, basi endelea kunegotiate. Usifanye hasira. Timiza masharti ya wazazi wa binti. Good luck and God Bless you.

Anonymous said...

Mahali ni tatizo. Wazazi angalieni uchumi wa mtu ndipo mpange mahali. Mmemkosesha binti yenu mume.