Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, December 11, 2013

AZRA VUYO JACK MTOTO ALIYEZALIWA MAHABUSU NA ANAENDELEA KUKULIA MAHABUSU SASA ATIMIZA MIAKA 2 WAZAZI WAKE WATUHUMIWA KUKUTWA NA MADAWA YA KULEVYA

MTOTO AZRA VUYO JACK SASA ANAMIAKA 2 NA BADO ANAENDELEA KUKULIA MAHABUSU  
MTOTO AZRA VUYO JACK 2  AKIWA NA MWANDISHI WETU   JOSEPH MWAISANGO NJE YA MAHAKAMA WAKATI KESI YA WAZAZI WAKE IKIENDELEA KUSIKILIZWA
BABA NA MAMA AZRA WAKIWA NA MTOTO WAO WAKISUBIRI KUINGIA MAHAKAMANI HII PICHA NI YA MIAKA MIWILI ILIYOPITA 
MTOTO AZRA VUYO JACK AKIWA AMELALA HAPA ALIKUWA NA MIEZI 5
TAASISI zinazohusika na haki za binadamu, ukatili wa kijinsia pamoja na Haki za watoto zimeombwa kuingilia kati suala la watoto wanaopata mateso magerezani kutokana na wazazi wao kutumikia adhabu.

Mwito huo umetolewa na baadhi ya wananchi kufuatia kuwepo kwa watoto waliozaliwa Gerezani lakini hakuna hatua zilizochukuliwa za kuwatoa nje ya gereza watoto hao na badala yake wanaendelea kukulia humo.

Baadhi ya watoto waliozaliwa gerezani na kuendelea kuishi humo ni pamoja na Azra Vuyo Jack(2) ambaye ni mtoto wa Anastazia Cloete (29) raia wa Afrika kusini aliyekamatwa miaka miwili iliyopita akituhumiwa kukutwa na madawa ya kulevya.

Tangu kujifungua kwa mwanamke huyo hakuna juhudi zozote zilizofanywa na mamlaka zinazohusika za kumnusuru mtoto Azra(2) kutokana na adhabu anayoitumikia mzazi wake na kumkumba yeye ambapo baadhi ya wasamaria wema wameendelea kujitolea kupeleka chakula.

Emily Mwaituka mmoja wa wasamaria wema anayejitolea kumlea mtoto huyo kwa kupeleka maziwa na chakula amesema anachoshangaa ni mateso anayoyapata mtoto huyo kwa kuishi gerezani wakati taasisi na vituo vya kulelea watoto vipo.

Amesema kinachomshangaza ni hata Ubalozi wa Afrika kusini hapa nchini kukaa kimya na kushindwa kushughulikia suala la kumtoa mtoto gerezani hadi anafikisha miaka miwili huku bado kukiwa hakuna dalili za kumtoa.

Ameongeza kuwa ni vema angeruhusiwa kumlea nyumbani kwake badala ya kumwacha kuendelea kuishi gerezani ambako kutamwathiri mtoto huyo kisaikolojia kutokana na maisha yagerezani.

Amesema mtoto huyo angewasubiri wazazi wake nje ya gereza wakati kesi yao inayoendelea kusikilizwa katika Mahakama kuu kanda ya Mbeya kwa kulelewa na wasamaria wema kama Serikali imeshindwa kumsaidia.

Mbali na mtoto huyo mwingine ni mtoto wa Wilvina Mkandara ambaye alijifungua mtoto akiwa gerezani baada ya kuhukumiwa kwenda jela miaka 30 kutokana na kukutwa na hatia ambapo mtoto wake hadi sasa anaumri wa miezi sita.

Hata hivyo ni watoto wengi wanaozaliwa Gerezani pindi wazazi wao wakiwa wanatumikia adhabu kwa mujibu wa Sheria, Swali je Sheria zinasemaje kuhusu mtoto ambaye hana hatia kuendelea kuishi gerezani hata kama anapata huduma zote za msingi?

 Haki za Watoto, Unicef, na Taasisi za Dini mpo wapi kufuatilia na kujua ni watoto wangapi wanaathirika kisaikolojia kwa kutumikia adhabu za wazazi wao magerezani na kuchukua hatua stahiki za kuwanusuru na hali hiyo?

Aidha baadhi ya wadau wamekiomba Chama cha waandishi wa Habari wanawake Tanzania(TAMWA) ambao wamekuwa mstari wa mbele kutoa elimu kwa jamii kuepuka ukatili wa kijinsia na watoto kuingilia kati suala hilo.

Wamesema ni bora taasisi hiyo ikalishughulikia suala hilo mapema kabla ya watoto hawajaathirika na uwepo wao ndani ya magereza kutokana na kukosa baadhi ya huduma kama michezo na watoto wenzie na haki ya kusoma.

Na Mbeya yetu

2 comments:

King said...

Duu Huyu Emmily Mwaituka Namfahamu sana ni mpiganaji wa siku nyingi sana pale mbeya Duu Toka enzi za kwa mwambusi, Jua kali Enterprise Cinema Kwa Mzee Mafakala na yule na pale Community Center duu hebu weka picha yake nione alivyo sasa

Anonymous said...

Mtoto hana kosa kwanini awausaidie wazizi azabu zao wakati vitabu vya dini vinasama kila mtu atabeba uovu wake mwenyewe. Mapolisi mtatubu wapi hizo zambi hata shetani siku hiyo atawakana