Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, December 10, 2013

WAFANYAKAZI WA NMB TAWI LA MBALIZI ROAD MBEYA WATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA AMANI NSALAGA MBEYA


Meneja wa NMB tawi la Mbalizi road  Atupele  Mwakibete amesema wameamua kutoa msaada huo kwa sababu wao ni sehemu ya jamii.
“Tumeamua kutoa msaada huu kwa kuguswa na matatizo mbalimbali wanayokabiliana nao vituo vingi vya kulelea watoto hapa nchini katika harakati zetu za kuhahikisha watoto yatima wanapata mahitaji muhimu katika maisha yao ya kila siku,” amesema.
Watoto wakituo cha Amani pamoja na walezi wao wakipokea msaada wa chakula na vifaa vya shule toka kwa wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la mbalizi Mbeya
Baadhi ya wafanyakazi wa NMB wakitoa zawadi kwa walezi wa watoto hao kituoni hapo
Alex Masawe moja ya wafanyakazi wa NMB Mbeya akitoa maelezo mafupi ya msaada wa vitu walivyotoa kwa watoto hao
Msimamizi wa kituo hicho Mchungaji Bahati Pangani akishukuru wafanayakazi wa NMB kwa msaada wao waliyoutoa kwa watoto hao kuwa ni moyo wa upendo wa kuwajali watoto hao kuwa wengine waige mfano huo wa benki ya NMB
Watoto wa kituo cha Amani wakiwaimbia wimbo wafanyakazi wa NMB wimbo usemao maisha mazuri kuwa hata wao wanatamani kuwa na maisha mazuri na kupata elimu bora hivyo wanaomba msaada ilinaowaisha mazuri
Baadhi ya wafanayakazi wa NMB wakiwa makini kusikiliza wimbo wa watoto hao huku baadhi ya wafanyakazi hao wakitokwa na machozi kutokana na wimbo huo kuwa na ujumbe mzito

No comments: