Baadhi wa wachezaji wanaounda timu ya Darts Mkoa wa Mbeya, Raymond Mushi alisema mazoezi wanayoendelea kuyafanya pamoja na kikosi kilichoundwa wapinzani wajue watakuja Mbeya kutalii tu.
MASHINDANO ya mchezo wa vishale (Darts)
kitaifa yanatarajia kufanyika Mkoani Mbeya kuanzia Novemba 23 hadi Novemba 24,
mwaka huu.
Akizungumzia hali ya maandalizi ya
michuano hiyo, Mwenyekiti wa Darts Mkoa wa Mbeya, Weston Asisya alisema baada
ya kupokea mwaliko wa kuwa mwenyeji wa michuano hiyo kwa mwaka huu kutoka Darts
taifa tayari maandalizi ya viwanja yameshakamilika.
Alisema michuano hiyo itafanyika katika
ukumbi wa Hoteli ya Kiwira iliyopo Jijini Mbeya ambapo jumla ya Mbao za
kuchezea 12 zimeshafungwa tayari kwa mashindano.
Alisema Mbeya itakuwa mara ya pili
kuandaa mashindano kama hayo kitaifa ambapo mara ya kwanza yalifanyika mwaka
2010 na yalikuwa na mafanikio makubwa hali iliyowavutia kuandaa tena.
Alisema katika mashindano ya mwaka huu
yanatarajia kushirikisha mikoa 12 yenye timu za vishale ikiwa na wachezaji
zaidi ya 150 Wanawake kwa wanaume ambapo Mkoa wa Mbeya unatakiwa kuandaa timu
nne kama mwenyeji.
Alisema kutokana na ukubwa wa Mkoa wa
Mbeya wameteua Wilaya ya Rungwe kuwakilishwa kama mkoa ambao utaopaswa kuandaa
timu mbili huku Mbeya Mjini nao ukibakia na timu mbili.
Kwa upande wake katibu wa Chama hicho
Mkoa wa Mbeya, Anna Mwakabonga alisema mbali na maandalizi ya kitaifa pia timu
ya Mkoa imeandaliwa vizuri kuhakikisha inafanya vizuri ikiwa nyumbani.
Alisema wamejipanga vizuri kuhakikisha
timu ya mkoa inaibuka na ushindi mnono tofauti na mashindano ya mwaka jana
yaliyofanyika kitaifa Mkoani Mwanza ambapo timu ya Wanawake ya Mkoa wa Mbeya
iliibuka kidedea kwa kujinyakulia kombe la mshindi wa pili.
Baadhi wa wachezaji wanaounda timu ya
Darts Mkoa wa Mbeya, Raymond Mushi alisema mazoezi wanayoendelea kuyafanya
pamoja na kikosi kilichoundwa wapinzani wajue watakuja Mbeya kutalii tu.
Alisema wamejipanga kuhakikisha
wanachukua ubingwa katika kila raundi watakayocheza na kwamba wachezaji wengi
ni wazoezi na wamecheza vishale kwa muda mrefu hivyo hawaoni sababu ya
kushindwa.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment