MAHAKAMA kuu kanda ya Mbeya, imemwachia
huru mtuhumiwa aliyekuwa amehukumiwa kifungo cha maisha na viboko 10 na
kutumikia kifungo hicho tangu mwaka 1999 kwa kosa la ubakaji baada ya kukata
rufani.
Hukumu ya rufaa hiyo imetolewa na
Jaji wa Mahakama kuu kanda ya Mbeya, Samweli Karua, baada ya rufaa
iliyowasilishwa mahakamani hapo namba 17 ya mwaka 2013, ambapo mtuhumiwa Isack
Righton(34) ameachiwa huru kutokana na vegozi vya hukumu dhidi yake kukiuka
baadhi ya vifungu.
Awali akisoma maelezo ya kosa la
Mtuhumiwa huyo, Mwendesha mashtaka wa Serikali, Ahmed Sitambuli alisema
mtuhumiwa huyo alifikishwa mbele ya mahakama ya Wilaya ya Mbozi Juni 1, 1999
akituhumiwa kutenda kosa la ubakaji kinyume na kifungu cha 130 na 131 (3) sura
ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Alisema mtuhumiwa huyo alidaiwa kutenda
kosa hilo April 4, 1999 wakati huo akiwa na miaka 20 baada ya mhanga wa tukio
hilo(jina limehifadhiwa) ambaye alikuwa anaishi na wazazi wake wakiwa wapangaji
katika nyumba iliyokuwa ikimilikiwa na mtuhumiwa huyo.
Ilidaiwa kuwa siku ya tukio
lililofanyika katika kijiji cha Kaloleni Tnduma wilayani Momba majira ya saa
moja jioni, wazazi wa Mhanga walikuwa wamemwacha binti yao nyumbani ili hali
wao wakiwa shambani ambapo baada ya kurudi walimsikia binti yao akilia huku
akitokea chumbani kwa mtuhumiwa na kumkuta akiwa na damu pamoja na mbegu za
kiume sehemu zake siri baada ya kufanyiwa uchunguzi.
Hata hivyo katika hukumu ya Jaji Karua
katika rufaa ya mtuhumiwa huyo, amesema hukumu iliyokuwa imetolewa na Hakimu wa
Mahakama ya Wilaya ya Mbozi, FCP Mdendemi ilikuwa na makosa ya kiushahidi.
Alisema hukumu hiyo ilikuwa na makosa
matatu ambayo aliyataja kuwa ni uwasilishaji wa kielelezo ambacho ni Fomu namba
tatu ya Polisi(Pf3) kuwasilishwa mbele ya mahakama na shahidi ambaye ni
mzazi wa mhanga Moses Simwanza badala ya Daktari aliyemfanyia uchunguzi.
Aliitaja sababu ya pili kuwa ni pamoja
na binti aliyefanyiwa kitendo hicho kushindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi
jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa ushahidi huku sababu ya tatu ikiwa ni
ushahidi uliotolewa mahamani hapo kuwa haukutosheleza kumtia hatiani mtuhumiwa
kwa sababu ya kutolewa na mashahidi watatu ambao ni baba mzazi wa mhanga, mama
mzazi na Askari Polisi Wp 381 Sajent Neema.
Kutokana na maelezo hayo Jaji karua
amemwachia huru mshtakiwa huyo ingawa amesota gerezaji kwa miaka 14 tangu
kuhukumiwa, ingawa mtuhumiwa huyo katika maelezo yake alikana kuhusika na tukio
hilo na kwamba hakuwepo eneo la tukio.
Na Mbeya yetu
|
2 comments:
Law as it is
Kwa wenzetu jamaa wangempa fidia.kasota na kupoteza mda mwingi.Duuuuuu
Post a Comment