Mlemavu wa Viungo, Damas Sanga(48) mkazi wa Igurusi Wilayani Mbarali Mkoa wa Mbeya wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutwa akiomba msaada katika baadhi ya Ofisi Mkoani Jijini hapa.
JAMII imetakiwa kutowaficha watu wenye
ulemavu bali iwajengee uwezo wa kufanya kazi kwa kuwatengea maeneo na siyo
kuwaacha wakiwa omba omba mitaani na wengine kufungiwa majumbani.
Rai hiyo imetolewa jana na Mlemavu wa
Viungo, Damas Sanga(48) mkazi wa Igurusi Wilayani Mbarali Mkoa wa Mbeya wakati
akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutwa akiomba msaada katika
baadhi ya Ofisi Mkoani Jijini hapa.
Sanga alisema si kila mlemavu anastahili
kubweteka na kusubiri kupewa misaada na kuomba omba mitaani bali wengine
wanauwezo wa kufanya kazi za ujasiliamali kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa
kiakili.
Alisema hivi sasa yeye binafsi anauwezo
wa kufanya kazi ya ufundi vyuma hivyo ameamua kuomba msaada ili aweze kununua
baadhi ya vifaa vitakavyomsaidia katika kazi yake hiyo ili aondokane na kuwa
tegemezi kwa kujitafutia riziki yake yeye mwenyewe.
Alivitaja baadhi ya vifaa
vinavyohitajika kuwa ni pamoja na Jenereta kubwa, Inveta na Kabwe kwa ajili ya
shughuli ya kuchomelea vitu vinavyogharimu Shilingi 390,000 ambapo hadi sasa
amefanikiwa kupata shilingi 290,000 alizochangiwa na wasamaria wema hivyo
kubakiwa na Shilingi 100,000/= tu.
Mjasiliamali huyo mwenye ulemavu wa
miguu alisema hivi sasa anafamilia ya mke mmoja na watoto wanne ambao hawezi kuwahudumia
bila kuwa na kazi ya kumwingizia kipato na ndiyo maana anaomba msaada ili aweze
kuendesha shughuli zake na kujipatia kipato kitakachoweza kuhudumia familia.
Alisema kwa mtu yeyote atakayeguswa na
hali yake awasiliane naye kwa simu namba 0764 036150 au afike nyumbani kwake
Shule ya Msingi Igurusi Wilayani Mbarali Mkoani hapa kwa msaada wa hali na
mali.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment