Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, November 26, 2013

KINANA ASHIRIKI NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA RUNGWE MASHARIKI.



 Ndugu Kinana na Ujumbe wake wakipita kukagua jengo la Maabara katika shule ya  sekondari ya Mwakaleli,katika halmashauri ya Busokelo,Wilayani Rungwe mkoani Mbeya.Mradi huo wa ujenzi wa madarasa na maabara ni  mpango serikali  wa kuboresha shule za sekondari zilizopo kwenye kata na Taifa kwa ujumla kwa kushirikiana na benki ya Dunia.
 Pichani chini, Ndugu Kinana akiwa amebeba tofali ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa ujenzi wa madarasa katika  shule ya  sekondari ya Mwakaleli,katika Halmashauri ya Busokelo,wilayani Rungwe.

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba za Walimu wa Shule ya Sekondari ya Mwakaleli.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Katende,katika halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe,mkoani Mbeya,Kinana aliwaeleza kuwa CCM inatekeleza ilani yake ya uchaguzi na kuongeza kuwa ahadi zilizoahidiwa zitatimizwa. Aidha Kinana alikazi pia kuwa kama chama Imara lazima kihoji serikali juu ya  pesa za ujenzi maendeleo ya wananchi,kwa nini hazitolewi kwa wakati. Ndugu Kinana yupo mkoani Mbeya kwa zaiara ya siku 11 katika kutekeleza Ilani ya CCM,kukagua miradi mbalimbali ikiwemo na kujua matatizo ama kero za Wanachi.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Katende  ndani ya halmshauri ya Busokelo wilayani Rungwe mkoani Mbeya,ambapo Nape aliwatahadharisha wakaji wa mji huo kuwa makini na vyama vinavyojita vya siasa,kutokana na kuanza kupoteza dira na muelekeo.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akikata ubao akiwa pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya maabara na madarasa ya shule ya Sekondari ya Mwakaleli.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na wazee wa kijiji ambao leo walimpa heshima ya kuwa Mzee wa Katende na kumvisha mgolole kama heshima ya mtu mzima.
 Katibu wa NEC Siasa na Mahusiano ya Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwa ameketi kwenye mkeka unaojulikana kama Kalili aliopewa zawadi na wakina mama wa Katende,Wilayani Rungwe mkoani Mbeya.
 Mzee Issa Simion akitoa salaam kwa niaba ya wazee wa Kijiji cha Katende na pia kushukuru kwa Serikali na Chama Cha mapinduzi na pia kuelezea kero zinazohusu wakazi wa kata ya Katende.
Mbunge wa Wanawake Mkoa wa Mbeya  Dk.Mary Mwanjelwa akiwasalimia wakazi Katende.katika halmashauri ya Busokelo,wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

No comments: