Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, October 28, 2013

WATU watano wamefariki dunia na wengine 22 kujeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka na kuharibika, baada ya dereva kushindwa kulimudu kutokana na mwendokasi. Songwe Mbeya

Kondakta wa basi hilo, Ulimboka Noah (26) alisema sababu ya kutokea kwa ajali hiyo ni kutokana na gari kugoma kubalisha gia ambapo dereva alivyojaribu kubadili ilishindikana ndipo alipojaribu kushuka nalo hivyo hivyo lakini kabla ya kufika darajani ilikuwa kama kitu kimelichota gari na kupinduka.
Muuguzi mkuu wa Hospitali Teule ya Ifisi ambako majeruhi wote walipelekwa, Sikitu Mbilinyi alikiri kupokea majeruhi 22 na kusema kati yao Wanaume 8 ambao hali zao zinaendelea vizuri kutokana na kutoumia sana ingawa wanamichubuko usoni na sehemu za mikono na miguu.



WATU watano wamefariki dunia na wengine 22 kujeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka na kuharibika, baada ya dereva kushindwa kulimudu kutokana na mwendokasi.

Ajali hiyo ilitokea  majira ya saa sita mchana katika Mtelemko wa Mlima Senjele katika Mpaka wa Halmashauri ya Mbeya na Wilaya ya Mbozi eneo la Songwe Mkoani hapa, wakati gari hilo likitokea Tunduma kwenda Jijini Mbeya.

Gari hilo lenye namba za usajili T 378 ADR aina ya Toyota Costa  lilikuwa likiendeshwa na Dereva Semu Mwakajwanga anayekadiliwa kuwa na umri kati ya miaka 60 na 70 ambaye alitoweka baada ya tukio.

Muuguzi mkuu wa Hospitali Teule ya Ifisi ambako majeruhi wote walipelekwa, Sikitu Mbilinyi alikiri kupokea majeruhi 22 na kusema kati yao Wanaume 8 ambao hali zao zinaendelea vizuri kutokana na kutoumia sana ingawa wanamichubuko usoni na sehemu za mikono na miguu.

Aliongeza kuwa kati ya majeruhi hao wanawake 10 walipokelewa wakiwa katika hali ya kuumia sana na kupatiwa matibabu ambapo kati yao Wanne walipewa Rufaa kutokana na hali zao kutokuwa katika hali nzuri, wengi wao wakiwa wameumia vichwa na kuvunjika miguu.

Alisema pia kati ya majeruhi hao watoto ni wanne ambao hali zao zinaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu na kuongeza kuwa taarifa za eneo la tukio kwamba watu wanne walikufa papo hapo na mtoto mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka mitano.

Kwa upande wake Kondakta wa basi hilo, Ulimboka Noah (26) alisema sababu ya kutokea kwa ajali hiyo ni kutokana na gari kugoma kubalisha gia ambapo dereva alivyojaribui kubadili ilishindikana ndipo alipojaribu kushuka nalo hivyo hivyo lakini kabla ya kufika darajani ilikuwa kama kitu kimelichota gari na kupinduka.

Alisema kutokana na jinsi lilivyopinduka gari hilo inasemekana ni kutokana na kukatika kwa Propela Shafti ambayo ilijikita chini kasha kupindua gari au U- Bolt inaweza ikawa imeachia kwa kile alichosema eneo lilikuwa zuri na hukuna kitu kilicholigusa gari hadi likapinduka.

Bado miili ya marehemu haijatambuliwa na imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Mbeya Ifisi. 

Na Mbeya yetu

1 comment:

Anonymous said...

Umesema propeler shaft au U- Bolt. Sisi wotae ni madereva, vipi kuhusu breki, zilikuwa sawa?