Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, October 30, 2013

WANAOTUPA WATOTO MAJALALANI NA VYOONI WAPEWA UJUMBE MZITO. MBEYA

Joseph Mwaisango Mwandishi wa Mbeya yetu akimpatia kiasi kidogo cha hela Rebeka kwa ajili ya kumnunulia mtoto chakula Mwandish wetu akiongea na Rebeca

Rebeca huyoo na mtoto wakeMwanamke mmoja anayesadikika kuwa na ulemavu wa akili aliyejitambulisha kwa jina  la Rebeka Mbwiga au mama Japhet amewatupia lawama wanawake wenye akilitimamu wanaozaa watoto na kushindwa kwalea.

Hayo amesema wakati akihojiwa na mwandishi wetu kuhusu mwanaume aliyemzalisha ili hali yeye ni kichaa ndipo alipojibu kuwa vichaa hawazai kwani yeye ameweza kuzaa na kutunza mtoto hivyo kichaa ni Yule mwenye akili timamu lakini anazaa na kutupa mtoto.

Amesema  hamfahamu aliyemzalisha huku wengine wakimkataza kuwataja kwa madai ya kuficha aibu kutokana na kuzaa na mlemavu wa akili lakini anauwezo wa kutunza watoto wake kwa kuomba misaada mitaani.

Ameongeza kuwa hadi sasa amezalishwa watoto sita na wanaume tofauti tofauti na wote wanaishi vizuri na hakuwatupa kama wanawake wengine wanavyofanya ingawa wanauwezo mzuri wa kiakili na fedha.

Na Mbeya yetu

No comments: