Ndege kubwa ya Fastjet ikiwa inaonekana angani wakati ikifanya survey juu ya uwanja wa kimataifa wa Songwe Mbeya
Hizi ni Ngazi maalum kabisa ambazo zinatarajiwa kutumika wakati ndege ya Fastjet itakapo anza safari zake mkoani Mbeya.
Wanaosalimiana ni Watumishi wa Eneo la uwanja wa Ndege na Aliye vaa Nguo za Blue pamoja ni Bwana Mwaipopo mdau mkubwa wa Mbeya yetu Blog.
Huyu Bwana mdogo anaitwa Eric Mwaisango nae alikuwepo kushuhudia ndege ya Fastjet
Hili ni eneo la Nje ya la Uwanja wa kimataifa wa Songwe Mbeya
****
Leo asubuhi majira ya saa Mbili na nusu Ndege ya Fastjet kwa Mara ya kwanza kabisa ilishuhudiwa na watu wachache katika Uwanja wa wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe ambapo ilikuwa ikifanya Survey angani bila kutua.
Ndege hiyo ambayo ilipita jirani kabisa na uwanja huo kwa Takribani ya zaidi ya mara tatu , ilifanya hivyo kwa sababu za kitaalam, hata hivyo hiyo ilikuwa ni amsha amsha huku siku chache zijazo ndege hiyo itatua kwa mara ya kwanza na Rasmi Jijini Mbeya katika uwanja wa Ndege wa Songwe.
Kwa nyakati Tofauti Baadhi ya Abiria waliokuwa wakijiandaa na kusafiri katika uwanja huo na Ndege zengine walionekana kuwa na furaha na kuzungumza mambo tofauti ikiwa na pamoja na kufurahishwa na hatua ya Ndege ya fastjet kuanza safari zake mkoani Mbeya na kusisitiza kwamba itakuwa ni Mkombozi mkubwa kutokana na bei zao kuwa chini na safari za uhakika.
Timu nzima ya Mbeya yetu Blog ilifika uwanjani mapema na kushuhudia kile kilicho onekana uwanjani hapo, na mpaka wanaondoka uwanjani hapo ndege hiyo ilikuwa tayari imesha anza safari za kurejea jijini Dar es salaam.
Je Mwananchi na Mkazi wa Mbeya na Mikoa ya Jirani unasemaje kuhusiana na Fastjet kuanza safari za kuja Mbeya hivi karibuni???
1 comment:
Ujio wa fasjet ni hatua kubwa ya kimeandeleo kwa mkoa wa Mbeya. Ni vema wananchi wakachangamkia na kuiunga mkono.
Post a Comment