Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, October 29, 2013

KITUO CHA RADIO ROCK FM 96.9 MBEYA CHASHEREHEKEA KUTIMIZA MIAKA MITATU NA KUTOA ZAWADI KWA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA TUMAINI UYOLE MBEYA

Mkurugenzi wa kituo cha ROCK FM 96.6 Allen Ezekia akiwakabidhi zawadi watoto wa kituo cha tumaini 

BABA MZAZI LAWENA NSONDA ambae pia alikuwa mgeni rasmi katika sherehe ya kutimiza miaka 3 ya kituo cha ROCK FM akikabidhi zawadi wa watoto wa kituo hicho cha tumaini pia LAWENA alitoa zawati ya vyereheni viwili vya kushonea nguo katika kituo hicho
Mkurugenzi wa kituo cha Tumaini Elias Katani akipokea zawadi kwa niaba ya watoto wa kituo chake toka kwa mkurugenzi wa ROCK FM ya jijini Mbeya
Watoto wa kituo cha tumaini wakishukuru kwa zawadi walizopewa na kituo cha ROCK FM
Lawena Nsonda amewatka wadau mbali mbali kujitokeza kuwasaidia watoto yatima kwani ni jukumu letu sote katika kuwalea
Mkurugenzi wa kituo cha Tumaini Elias Katani akishukuru kwaniaba ya watoto kwa zawadi walizopatiwa na Rock Fm 96.6 
Mratibu Elimu kituo hicho Obadia Mbilinyi akisoma taarifa fupi ya kituo hicho cha Tumaini
Mara baada ya kutoka toa zawadi kwa watoto yatima sherehe iliendelea katika viwanja vya TIA Mbeya
Moja ya watangazaji wa Rock Fm Harubu Kabwe akimkaribisha mkurugenzi wake aje apate keki katika sherehe hiyo
BABA MZAZI LAWENA NSONDA akimlisha keki mkurugenzi wa ROCK FM 96.9 Allen Ezekia katika sherehe ya kutimia miaka 3 sherehe zilizofanyka katika uwanja wa chuo cha TIA Mbeya
Mkurugenzi wa kituo cha ROCK FM 96.6 Allen Ezekia akiwashukuru wasikilizaji wa Rock fm waliojitokeza katika sherehe hiyo ya kutimiza miaka 3 na kuwaahidi kuwa watazidi kuwaletea habari za uhakika na kuburudisha
 Mgeni rasmi katika sherehe hiyo BABA MZAZI LAWENA NSONDA akiwahutubia wananchi waliohudhuria sherehe za kutimia miaka 3 ya kituo cha ROCK FM 96.9 
Burudani mbali mbali zilikuwepo katika sherehe hiyo ya kutimiza miaka 3 ya ROCK FM 96.9 
Dachi Nationale Band wakitumbuiza katika sherehe ya kutimiza miaka 3 ya ROCK FM 96.9
Watangazaji wa kituo cha Radio ROCK FM 96.9 wakiwa katika picha ya pamoja

Na Mbeya yetu

No comments: