Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, September 4, 2013

TIMU YA NETBOLI YA FILBERT BAYI YA JIJINI DAR ES SALAAM YAFANIKIWA KUTETEA UBINGWA WA LIGI DARAJA LA KWANZA KWA MARA YA PILI MFULULIZO.

Timu ya Filbert Bay
Timu ya JKT Bweni
Naibu waziri Mulugo akienda kukagua timu
Timu zikiwajibika uwanjani
Mgeni rasmi wa siku ya kufunga Ligi ya Netboli, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo akihutubia katika kilele cha ligi ya Netboli daraja la kwanza 
Mwenyekiti  wa Chaneta taifa Annah Kibira akiwahutubia wachezaji na mashabiki waliokuwepo uwanjani kwenye kufunga ligi
Katibu wa Chaneta taifa,Maimuna Mrisha akitangaza msimamo wa ligi baada ya kukamilika 
Mashabiki wakishangili ushindi uwanjani hapo

Timu ya mpira wa Pete ya Filbert Bayi ya Kutoka Dar Es Salaam imefanikiwa kunyakua ubingwa wa Ligi daraja la Kwanza msimu wa 2013 kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuwachabanga wapinzani wao kwa  bila huruma.

Timu hiyo imefanikiwa kuchukua ubingwa katika ligi iliyoanza Agosti 28, Mwaka huu na kukamilika Septemba Mosi, Mwaka huu na kuzikutanisha timu za Netboli 12 kutoka maeneo mbali mbali, ligi iliyokuwa ikifanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Mkoani Mbeya.

Timu ya Filbert Bayi ambayo mchezo wa Mwisho ilicheza na timu ya Jkt Mbweni katika mchezo uliokuwa na upinzani mkali ambapo Filibert Bayi walifanikiwa kuondoka na pointi zote baada ya kuwachabanga wapinzani wao kwa jumla ya magoli 22 kwa 21.

Hadi mwisho wa Ligi hiyotimu ya Filbert Bayi ilikuwa ikiiongoza ligi ikiwa na alama 22 huku ikiwa imecheza michezo 11 na kufunga magoli 391 huku ikiruhusu magoli 181 katika lango lao kutoka katika timu zote.

Akitangaza msimamo wa ligi hiyo katika fainali zilizofanyika katika Uwanja wa Sokoine na kufungwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, Katibu wa Chaneta Taifa, Maimuna Mrisha amesema timu zote zilikuwa na upinzani mkubwa hali inayoonesha maandalizi yalikuwa maziri.

Naye Katibu wa Chaneta Mkoa wa Mbeya, Pudensiana Baitu amaesema michuano ya mwaka huu ilikuwa inakabiliwa na changamoto ya fedhaambayo imesababishwa na makampuni kutokuwa wazi pindi wanapoombwa michango.

Amesema bajeti ya michuano hiyo ilikuwa Milioni 16,400,000 lakini fedha amazo zilikuwa zimekusanywa zilifikia Milioni 2,500,000 hadi ligi inaisha hivyo kubakiza deni la shilingi  Milioni 1,200,000.

Aidha kufuatia uwepo wa deni hilo Katibu huyo amesema wamejitahidi kujibana lakini fedha hiyo ilitakiwa kulipia malazi kwa viongozi wa Chaneta taifa ambapo  deni hilo lililipwa papo hapo baada ya Mc wa shughuli ya ufungaji Charles Mwakipesile kuchangisha fedha hizo kutoka kwa wageni waliohudhuria ambalo lilipwa na Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Musa Zungiza, Mkurugenzi wa Filbert Bayi, Afisa Uhamiajiwa Mkoa wa Mbeya na Mwakipesile.

Mwenyeki wa Chaneta Taifa, Annah Kibira alitangaza kuwa timu zote zilizoshiriki ligi daraja la kwanza msimu huu hakuna timu itakayoshuka daraja hivyo zote zitaendelea kubaki ligi daraja la kwanza.

Na huu ndiyo msimamo wa ligi hiyo.

TIMU
IDADI YA MICHEZO
MAGOLI ALIYOFUNGA
MAGOLI ALIYOFUNGWA
ALAMA
Filbert Bay
11
391
181
22
JKT Mbweni
11
401
185
20
Magereza Morogoro
11
352
249
17
Jeshi Star
11
311
217
17
Hamambe
11
332
299
13
Uhamiaji
11
283
258
13
JKT Ruvu
11
280
309
9
Polisi Arusha
11
196
272
8
TTPL Morogoro
11
258
322
7
Polisi Mwanza
11
243
316
4
Polisi Mbeya
11
166
376
2
CMTU Dsm
11
185
365
0



Na Mbeya yetu 

No comments: