SERIKALI kupitia kitengo cha Ustawi wa Jamii
imetakiwa kuzisimamia na kuzikagua baadhi ya Asasi ili kuzijua uhalali wake
kutokana na kutokufanya kulingana na malengo ya usajili wake katika jamii.
Imeelezwa kuwa Asilimia kubwa ya Asasi
hizo zinafanya kazi ya kujiingizia kipato tofauti na hali halisi ya usajili
wake ambao ni kuisadia jamii ili kuondokana na Umaskini na kuongeza vipato
vyao.
Hayo yamebainishwa leo na Mkurugenzi mtendaji wa
Shirika la Women & Youth Development Society, Sophia Mwakagenda,
katika Mafunzo ya kuwajenga uwezo wa kuweka mali na kuongeza akiba kwa
wajasiliamali wa Jiji la Mbeya, mafunzo yanayofanyika katika ukumbi wa Kiwira
Motel.
Mwakagenda amesema baadhi ya Asasi hazifanyi
kile kilichokusudiwa katika jamii hivyo ni Vema Serikali ikawa na utaratibu wa
kuzikagua ili kujionea ufanisi wake na kama zinafanya kulingana na usajili wake
na siyo kukaa na kusubiria ripoti maofisini.
Amesema katika mafunzo yanayoendelea katika
ukumbi huo imeonekana kuwa na mwitikio mdogo uliotokana na baadhi ya Asasi
kufanya mafunzo yasiyokuwa na tija kwa Mjasiliamali ambapo hufanya mafunzo kwa
nia ya kujiingizia kipato na kuwaibia wananchi badala ya kuwaongezea kipato.
Amesema mafunzo hayo yatakuwa ya siku tatu
ambayo yatawasaidia wananchi jinsi ya kuweka akiba na kuongeza mali kutokana na
kubainika kuwa Wanawake wengi wanajiingiza katika mikopo ambayo huzidi
kuwaletea umaskini hivyo kupitia mafunzo hayo wataweza kufundishwa namna ya
kutumia fedha kwa nidhamu.
Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa mafunzo hayo
yanaendeshwa kwa ushirikiano wa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO),
benki ya CRDB, Bacrays na Cokacola ambapo mbali na mafunzo hayo wajasiliamali
hao watafundishwa pia namna ya utengenezaji wa bidhaa mbali mbali kama
mishumaa, batiki na Sabuni mafunzo yatakayodumu kwa siku tatu kuanzia Septemba
12 hadi Septemba 14, Mwaka huu.
|
No comments:
Post a Comment