Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, August 24, 2013

Wakazi wa wilaya ya Chunya wapo hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na Halmashauri ya wilaya kushindwa kuzoa taka katika ghuba la soko kuu wilayani humo.


Ghuba lililolundikwa taka sasa limekuwa malisho ya mifugoHili ndilo soko linaloendelea kujengwaWakazi wa wilaya ya Chunya wapo hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na Halmashauri ya wilaya kushindwa kuzoa taka katika ghuba la soko kuu wilayani humo.

Wakazi hao waliongea jinsi wanavyokerwa na hali hiyo kufuatia kujaa kwa taka na kushindwa kuzolewa kwa muda mrefu takribani mwezi mmoja licha ya kutozwa ushuru kila mwezi kati ya shilingi elfu tatu hadi elfu sita.

Ghuba hilo hivi sasa linatumiwa pia na wananchi wanaolizunguka soko hilo ingawa hawachangii tozo lolote na taka zimekuwa zikizagaa kwenye makazi ya watu na hata kwenye migahawa inayozunguka ghuba hilo.
Mwenyekiti wa soko hilo Bwana EMMANUEL MWAKAJUMBA alikataa kulizungumzia suala hilo licha ya kukiri kuwepo kwa taka hizo kwa muda mrefu sasa ingawa wafanyabiashara wamekuwa wakitozwa tozo ya usafi kila mwezi.

Aidha ujenzi wa soko hilo umeendelea baada ya kusimama kwa muda mrefu kutokana na ukosefu wa pesa ambapo sasa kiasi cha shilingi milioni sitini zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na awamu ya pili ya uezekajii wa mabati baada ya kukamilika kwa lenta.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya CHAKUPEWA MAKELELE Amesema kuwa nia ya Halmashauri yake ni kumaliza soko hilo kwa wakati kadri wanavyopata pesa ili kuwaondolea adha wakazi wa wilaya hiyo lakini pia kuongeza mapato ya Halmashauri.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Chunya DEODATUS KINAWIRO  amesema nia ya serikali ni kuhakikisha inaboresha kila maeneo ikiwa ni pamoja elimu ,afya,barabara kwa kutumia vyanzo vya mapato ya ndani ili kuwaletea wananchi maendeleo yaliyokusudiwa.

Picha na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu

No comments: