Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, August 24, 2013

Kikundi cha wachimbaji wadogo wa madini cha JIKOMBOE cha SAZA Wilayani CHUNYA kimeiomba serikali kutatua mgogoro unaohusu mlima ELIZABETH baina ya makampuni ya SHANTA na BAFEX uliodumu kwa miaka mitatu sasa.

Kulia naibu kamishina wa madini nchini John Nayopa akiwa na afisa madini wakiangalia vipimo katika mgodi mlima Elizabeth huko Saza Chunya
Maafisa madini na wachimbaji wakikagua vipimo katika mlima Elizabeth
Moja kati ya wachimbaji wadogowadogo akiwa na mwanae katika mlima Elizabeth
Baadhi ya wachimbaji wa kikundi cha jikomboe wakiambatana na maafisa madini kukagua eneo linalolalamikiwa
Naibu kamishna wa madini John Nayopa akihutubia wanakikundi cha jikomboe kushoto ni katibu tawala wilaya ya Chunya Sosten Mayoka kulia ni kamishna wa madini kanda ya Mbeya John Shija


Kikundi cha wachimbaji wadogo wa madini cha JIKOMBOE cha SAZA Wilayani CHUNYA kimeiomba serikali kutatua mgogoro unaohusu mlima ELIZABETH baina ya makampuni ya SHANTA na BAFEX uliodumu kwa miaka mitatu sasa.

Mwenyekiti wa kikundi cha JIKOMBOE ROBERT NSELU  amelalamika maamuzi ya wizara ya madini kuwapendelea wawekezaji.

Mgogoro huo umeshindwa kupatiwa ufumbuzi kutokana na mkanganyiko uliofanywa na maafisa wa madini wilaya ya CHUNYA baada ya kupokea maombi kutoka kikundi cha JIKOMBOE na kuridhia maombi yao kisha Wizara kuwapa leseni.

Mara baada ya kupewa leseni ya kumiliki mlima ELIZABETH kampuni ya BAFEX iliibuka na kudai kuwa hilo ni eneo lake kihalali na kuzua mtafaruku ambao ulipelekea mara kadhaa kujadiliwa na Afisa madini kanda Bwana JOHN SHIJA bila mafanikio.

SHIJA baada ya kushindwa kutatua mgogoro huo aliamua kuupeleka wizarani ambapo mara kadhaa wizara wameujadili bila kupatiwa ufumbuzi hali iliyopelekea wizara kumwagiza Naibu Kamishina wa Madini JOHN NAYOPA ili atatue suala hilo.

NAYOPA baada ya kutembelea mlima ELIZABETH alibaini makosa yaliyofanywa na maafisa madini kwa kutoa Hekta 71 badala ya 10 zinazotakiwa kisheria na isitoshe mchora ramani kuonesha kuwa ombi la TUJIKOMBOE ni la mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la JOSEPH MAKERERE.

Mbali ya hilo NAYOPA Amesema mchoro unaonesha kuwa kiwanja hicho kipo MBARALI badala ya SAZA CHUNYA kama kilivyoombwa na TUJIKOMBOE Hali ambayo NAYOPA inaashiria kuwepo mazingira ya rushwa.

Kuokana na utata huo NAYOPA Ameamua kuupeleka mgogoro huo kwa waziri wa madini ili aweze kutolea uamuzi ambao utakuwa hitimisho la mgogoro huo.

Wakati huo huo Kamishina wa kanda Bwana JOHN SHIJA amewapa fursa kikundi cha JIKOMBOE kuleta maombi ya ardhi ya kuchimba kwa vile wao ni kikundi hivyo atawapa kipau mbele kuhakikisha wanapata lesni kwa wakati.

Picha na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu

No comments: