Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, August 14, 2013

Serikali pamoja viongozi wa dini zote bado hawajampata adui anayevuruga amani ya nchi kwa misingi ya udini na Siasa.



Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Chrispin Meela akitoa Hotuba katika Msikiti Mkuu wa Mbeya kwa waumini wa Dini ya Kiislam wakati wa Baraza la Idd.
 Mmoja wa Viongozi wa Dini ya Kiislam akihutubia wakati wa Baraza la Eid

 Waumini Mbalimbali wa Dini ya Kiislam wakiwa katika Baraza la Idd

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Chrispin Meela wa pili kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Dini ya Kiislam

Imeelezwa kwamba Serikali  pamoja viongozi wa dini zote bado hawajampata adui anayevuruga amani ya nchi kwa misingi ya udini na Siasa.
 Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Mkoani Mbeya, Chrispin Meela, wakati akiwahutubia waumini wa dini ya  kiislamu kwenye baraza la Eid iliyofanyika hivi karibuni  katika msikiti mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Meela alisema kuwa hivi sasa nchi inavurugwa kwa misingi ya Udini na Siasa huku wanaokamatana uchawi wakiwa ni watanzania wenyewe bila ya kujua kiini cha mtu anayeanzisha vurugu hizo.
Alidai kuwa hali hiyo inawezekana kwamba kuna mkono wa mtu kutoka hata nje nchi anayetaka kuona nchi inakuwa haina amani na si vingenevyo.
“Viongozi wa dini zote, Serikali na viongozi wanasiasa ni lazima tukaye chini tutafakari kwa kiina  na kumtafuta mchawi anayetuvuruga badala ya kukamatana uchawi sisi kwa sisi na hapa lazima kuna mkono wa mtu mwingine na isitoshe anatoka hata nje ya nchi hasa tukirejea historia ya utamaduni wetu watanzania hatukwa na mvurugano kama huu wa sasa kwa miaka mingi iweje leo hii,” alisema Meela.
Alisema hivi sasa kinachofanyika kwa watanzania kulipizana visasi ambavyo hata havina ukweli wowote kwani akipigwa mwislamu kauli inatolewa kwamba ni mkristo ndiye aliyefanya hivyo na mkristo akipigwa eti mwislamu ndiye aliyehusika.
Hali kadharika Meela, alisema hata kwenye masuala ya Siasa mtindo mmoja ambapo vurugu zikitokea  katika mkutano wa Chadema basi CCM ndio waliofanya vurugu hizo ama zikitokea katika Mkutano wa CCM basi vivyo hivyo Chadema ndio chanzo.
Alisema kuwa bado kuna kazi ngumu kwa viongozi wa dini na Serikali ya kumtafuta adui anayetaka kuona nchi haitawaliki kwa misingi ya udini ama Siasa,  huku mkuu huyo wa Wilaya akiwasisitiza viongozi wa dini zote kuliombea taifa ili kuombana na kasumba hiyo mbaya na inayoichafua sura ya nchi na watanzania wake.

No comments: